Judges 12:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha watu wakavishika vivuko vya mto Yordani ili kuiziba njia ya watu wa Efraimu. Kila mara alipotokea mkimbizi akaomba kupita huko, watu wa Gileadi walimwuliza, “Je, wewe ni Mwefraimu?” Na kama alijibu, “La,”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wagileadi wakaviteka vivuko vya Mto Yordani kuelekea Efraimu. Kisha ilikuwa yeyote aliyenusurika kutoka Efraimu aliposema, “Niache nivuke,” hao wanaume wa Gileadi walimuuliza, “Je wewe ni Mwefraimu?” Akijibu “Hapana,”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao Wagileadi wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha hao Waefraimu; kisha ilikuwa, hapo watoro waliotoroka Efraimu mmojawapo aliposema Niache nivuke, hao watu wa Gileadi wakamwambia, Je! Wewe u Mwefraimu? Kwamba alisema, La;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha watu wakavishika vivuko vya mto Yordani ili kuiziba njia ya watu wa Efraimu. Kila mara alipotokea mkimbizi akaomba kupita huko, watu wa Gileadi walimwuliza, “Je, wewe ni Mwefraimu?” Na kama alijibu, “La,”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wagileadi wakaviteka vivuko vya Yordani dhidi ya hao Waefraimu, kisha ilikuwa ye yote yule aliyenusurika katika Efraimu aliposema, “Niache nivuke,” hao watu wa Gileadi walimwuliza, “Je wewe ni Mwefraimu?” Kama alijibu “Hapana,”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wagileadi wakaviteka vivuko vya Yordani dhidi ya hao Waefraimu, kisha ilikuwa yeyote yule aliyenusurika katika Efraimu aliposema, “Niache nivuke,” hao watu wa Gileadi walimuuliza, “Je wewe ni Mwefraimu?” Kama alijibu “Hapana,”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao Wagileadi wakavitwaa vivuko vya Yordani kinyume cha hao Waefraimu; kisha kila mmoja wa watoro walitoroka Efraimu aliposema “Niache nivuke”, hao watu wa Gileadi walimuuliza, “Je! Wewe ni Mwefraimu?” Alijibu, la;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha watu wakavishika vivuko vya mto Yordani ili kuiziba njia ya watu wa Efraimu. Kila mara alipotokea mkimbizi akaomba kupita huko, watu wa Gileadi walimwuliza, “Je, wewe ni Mwefraimu?” Na kama alijibu, “La,”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Wagileadi walivitwaa vivuko vya Yordani vya kwenda Efuraimu. Vikawa hivyo: kila mara watoro wa Efuraimu waliposema: Na nivuke, watu wa Gileadi wakamwuliza: Wewe u Mwefuraimu? Naye aliposema: Hapana,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao Wagileadi wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha hao Waefraimu; kisha ilikuwa, hapo watoro waliotoroka Efraimu mmojawapo aliposema Niache nivuke, hao watu wa Gileadi wakamwambia, Je! Wewe u Mwefraimu? Kwamba alisema, La;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha watu wakavishika vivuko vya muto Yordani kwa kuiziba njia ya watu wa Efuraimu. Kila mara mukimbizi alipotokea akiomba kupita kule, watu wa Gileadi walimwuliza: “Wewe ni Mwefuraimu?” Na kama akijibu “Hapana”,