Judges 12:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
walimwambia: “Haya tamka neno ‘Shibolethi’” lakini yeye hutamka “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kulitamka sawasawa. Hapo, walimkamata, wakamuua huko kwenye vivuko vya mto Yordani. Watu 42,000 wa Efraimu walipoteza maisha yao wakati huo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
walimwambia, “Sawa, sema ‘Shibolethi’.” Iwapo alitamka, “Sibolethi”, kwa sababu hakuweza kutamka hilo neno sawasawa, walimkamata na kumuua hapo kwenye vivuko vya Mto Yordani. Waefraimu elfu arobaini na mbili waliuawa wakati huo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo wakamwambia, Haya, tamka sasa neno hili, Shibolethi; naye akasema, Sibolethi; kwa maana hakuweza kufanya midomo yake kutamka neno hilo sawasawa; ndipo wakamshika, na kumwua hapo penye vivuko vya Yordani; basi wakaanguka wakati huo watu arobaini na mbili elfu wa Efraimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
walimwambia: “Haya tamka neno ‘Shibolethi;’” lakini yeye hutamka “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kulitamka sawasawa. Hapo, walimkamata, wakamuua huko kwenye vivuko vya mto Yordani. Watu 42,000 wa Efraimu walipoteza maisha yao wakati huo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
walimwambia, “Sawa, sema ‘Shibolethi.’ ” Iwapo alitamka, “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kutamka hilo neno sawasawa, walimkamata na kumwua hapo kwenye vivuko vya Yordani. Waefraimu 42,000 waliuawa wakati huo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
walimwambia, “Sawa, sema ‘Shibolethi.’ ” Iwapo alitamka, “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kutamka hilo neno sawasawa, walimkamata na kumuua hapo kwenye vivuko vya Yordani. Waefraimu 42,000 waliuawa wakati huo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo walipomwambia, Haya, tamka sasa neno hili, Shibolethi; naye akasema, Sibolethi; kwa maana hakuweza kufanya midomo yake kutamka neno hilo sawasawa; ndipo wakamshika, na kumwua hapo penye vivuko vya Yordani; basi wakaanguka watu elfu arobaini na mbili wa Efraimu wakati huo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
walimwambia: “Haya tamka neno ‘Shibolethi’” lakini yeye hutamka “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kulitamka sawasawa. Hapo, walimkamata, wakamuua huko kwenye vivuko vya mto Yordani. Watu 42,000 wa Efraimu walipoteza maisha yao wakati huo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakamwambia: Tamka Shiboleti! Tena aliposema: Siboleti kwa kuwa hakuweza kutamka Shiboleti, wakamkamata, wakamwua hapo penye vivuko vya Yordani; ndivyo, walivyouawa wakati huo Waefuraimu 42000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo wakamwambia, Haya, tamka sasa neno hili, Shibolethi; naye akasema, Sibolethi; kwa maana hakuweza kufanya midomo yake kutamka neno hilo sawasawa; ndipo wakamshika, na kumwua hapo penye vivuko vya Yordani; basi wakaanguka wakati huo watu arobaini na mbili elfu wa Efraimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
walimwambia: “Basi useme neno ‘Shiboleti’ ”. Lakini yeye akisema “Siboleti” kwa sababu hakuweza kulitamka sawasawa, walimukamata na kumwua kule kwenye vivuko vya muto Yordani. Watu elfu makumi ine na mbili wa Efuraimu wakapoteza maisha yao wakati ule.