Judges 13:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Manoa akafuatana naye mpaka kwa mtu huyo, akamwuliza, “Je, wewe ni yule mtu aliyezungumza na mwanamke huyu?” Yule mtu akamjibu, “Ni mimi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Manoa akainuka akaandamana na mkewe. Alipomfikia yule mtu akamuuliza, “Je, wewe ndiwe ulisema na mke wangu?” Akasema, “Ni mimi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Manoa akainuka, akamwandama mkewe, na kumfikilia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Naam, ni mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Manoa akafuatana naye mpaka kwa mtu huyo, akamwuliza, “Je, wewe ni yule mtu aliyezungumza na mwanamke huyu?” Yule mtu akamjibu, “Ni mimi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Manoa akainuka akaandamana na mkewe. Alipomfikia yule mtu akamwuliza, “Je, wewe ndiye yule uliyesema na mke wangu?” Akasema, “Mimi ndiye.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Manoa akainuka akaandamana na mkewe. Alipomfikia yule mtu akamuuliza, “Je, wewe ndiye yule uliyesema na mke wangu?” Akasema, “Mimi ndiye.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Manoa akainuka, akamfuata mkewe, na kumfikia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Ndio, ni mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Manoa akafuatana naye mpaka kwa mtu huyo, akamwuliza, “Je, wewe ni yule mtu aliyezungumza na mwanamke huyu?” Yule mtu akamjibu, “Ni mimi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Manoa alipoondoka, akamfuata mkewe, akafika kwa yule mtu, akamwuliza: Wewe ndiwe yule mtu aliyesema na huyu mwanamke? Akasema: Ni mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Manoa akainuka, akamwandama mkewe, na kumfikilia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Naam, ni mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Manoa akafuatana naye mpaka kwa mutu huyo, akamwuliza: “Wewe ni yule mutu aliyezungumuza na mwanamuke huyu?” Yule mutu akamujibu: “Ni mimi.”