Judges 13:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia Manoa, “Hata kama mkinilazimisha kukaa sitakula chakula chenu. Lakini kama ukipenda, tayarisha sadaka ya kuteketezwa, mtolee Mwenyezi-Mungu.” Manoa hakujua kuwa huyo alikuwa malaika wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wa Mwenyezi Mungu akamjibu, “Hata kama utanizuia, sitakula chochote kwako. Lakini ukitaka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, mtolee Mwenyezi Mungu.” (Manoa hakumtambua kuwa huyu alikuwa malaika wa Mwenyezi Mungu.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini malaika wa Bwana akamwambia Manoa, Ujapokuwa wanizuia, sitakula katika mkate wako; na kwamba wataka kufanya tayari sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsongezea Bwana. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia Manoa, “Hata kama mkinilazimisha kukaa sitakula chakula chenu. Lakini kama ukipenda, tayarisha sadaka ya kuteketezwa, mtolee Mwenyezi-Mungu.” Manoa hakujua kuwa huyo alikuwa malaika wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wa BWANA akamjibu, “Hata kama utanizuia, sitakula cho chote kwako. Lakini ukitaka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, mtolee BWANA hiyo sadaka.” (Kwa kuwa Manoa hakujua kuwa alikuwa malaika wa BWANA.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wa bwana akamjibu, “Hata kama utanizuia, sitakula chochote kwako. Lakini ukitaka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, mtolee bwana hiyo sadaka.” (Kwa kuwa Manoa hakujua kuwa alikuwa malaika wa bwana.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini malaika wa BWANA akamwambia Manoa, “Ijapokuwa unanizuia, sitakula chakula chako; lakini kama unataka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsogezea BWANA”. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia Manoa, “Hata kama mkinilazimisha kukaa sitakula chakula chenu. Lakini kama ukipenda, tayarisha sadaka ya kuteketezwa, mtolee Mwenyezi-Mungu.” Manoa hakujua kuwa huyo alikuwa malaika wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini malaika wa Bwana akamwambia Manoa: Ijapo unishike, sitakila chakula chako; lakini ukitaka kutoa ng'ombe ya tambiko, mtolee Bwana ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima. Kwani Manoa hakujua, ya kuwa yeye ni malaika wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini malaika wa BWANA akamwambia Manoa, Ujapokuwa wanizuia, sitakula katika mkate wako; na kwamba wataka kufanya tayari sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsongezea BWANA. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule malaika wa Yawe akamwambia Manoa: “Hata kama mukinilazimisha kukaa, sitakula chakula chenu. Lakini kama ukipenda, tayarisha sadaka ya kuteketezwa kwa moto, umutolee Yawe.” Manoa hakujua kwamba huyo alikuwa malaika wa Yawe.