Judges 13:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mkewe akamjibu, “Kama Mwenyezi-Mungu angetaka kutuua hangepokea sadaka yetu ya kuteketezwa na ya nafaka; wala hangetuonesha mambo hayo wala kutuambia maagizo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mkewe akamwambia, “Ikiwa Mwenyezi Mungu alikuwa amekusudia kutuua, hangepokea sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya unga kutoka mikononi mwetu, wala hangetuonesha mambo haya yote wala kututangazia mambo haya wakati huu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mkewe akamwambia, Kama Bwana angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonyesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mkewe akamjibu, “Kama Mwenyezi-Mungu angetaka kutuua hangepokea sadaka yetu ya kuteketezwa na ya nafaka; wala hangetuonesha mambo hayo wala kutuambia maagizo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mkewe akamwambia, “Ikiwa BWANA alikuwa amekusudia kutuua, asingelipokea sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya unga kutoka mikononi mwetu, wala asingelituonyesha mambo haya yote wala kututangazia mambo kama haya wakati huu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mkewe akamwambia, “Ikiwa bwana alikuwa amekusudia kutuua, asingelipokea sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya unga kutoka mikononi mwetu, wala asingelituonyesha mambo haya yote wala kututangazia mambo kama haya wakati huu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mkewe akamwambia, Kama BWANA angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mkewe akamjibu, “Kama Mwenyezi-Mungu angetaka kutuua hangepokea sadaka yetu ya kuteketezwa na ya nafaka; wala hangetuonesha mambo hayo wala kutuambia maagizo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mkewe akamwambia: Kama Mungu angependa kutuua, asingalipokea mikononi mwetu ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima pamoja na kilaji cha tambiko, wala asingalituonyesha hayo yote, wala asingalitupasha habari hizo zote wakati huo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mkewe akamwambia, Kama BWANA angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonyesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini muke wake akamujibu: “Kama Yawe angetaka kutuua hangepokea sadaka yetu ya kuteketezwa kwa moto na ya ngano; wala hangetuonyesha mambo hayo wala kutuambia maagizo.”