Judges 13:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini aliniambia kwamba nitachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume. Aliniamuru nisinywe divai au kileo wala kula chochote kilicho najisi, maana mtoto huyo atakuwa amewekwa wakfu kwa Mungu tangu kuzaliwa kwake mpaka atakapokufa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini aliniambia, ‘Utachukua mimba na utazaa mtoto wa kiume. Basi sasa, usinywe divai wala kileo kingine chochote, wala usile kitu kilicho najisi, kwa kuwa huyo mtoto atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yake hadi kufa kwake.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini aliniambia kwamba nitachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume. Aliniamuru nisinywe divai au kileo wala kula chochote kilicho najisi, maana mtoto huyo atakuwa amewekwa wakfu kwa Mungu tangu kuzaliwa kwake mpaka atakapokufa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini aliniambia, ‘Utachukua mimba na utazaa mtoto mwanaume. Basi sasa, usinywe mvinyo wala kileo kingine cho chote wala usile kitu kilicho najisi, kwa kuwa huyo mtoto atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yake mpaka kufa kwake.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini aliniambia, ‘Utachukua mimba na utazaa mtoto mwanaume. Basi sasa, usinywe mvinyo wala kileo kingine chochote wala usile kitu kilicho najisi, kwa kuwa huyo mtoto atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yake mpaka kufa kwake.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utazaa mtoto wa kiume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hadi siku ya kufa kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini aliniambia kwamba nitachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume. Aliniamuru nisinywe divai au kileo wala kula chochote kilicho najisi, maana mtoto huyo atakuwa amewekwa wakfu kwa Mungu tangu kuzaliwa kwake mpaka atakapokufa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaniambia: Utajiona kuwa mweye mimba, kisha utazaa mtoto mwanamume. Toka sasa usinywe mvinyo wala kileo cho chote, wala usile chakula cho chote chenye mwiko, kwani kijana huyo atakuwa ametengwa kuwa wake Mungu tangu hapo, atakapozaliwa hata siku ya kufa kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini aliniambia kwamba nitabeba mimba na kuzaa mutoto mwanaume. Aliniamuru nisikunywe divai au kileo wala kula chochote kinachohesabiwa kuwa kichafu, maana mutoto huyo atakuwa Munaziri wa Mungu tangu kuzaliwa kwake mpaka atakapokufa.”