Judges 14:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Samsoni akawaambia, “Nitatega kitendawili. Kama mkiweza kutegua kitendawili hicho kwa muda wa siku saba za sherehe za harusi, basi, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi thelathini ya sikukuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Samsoni akawaambia, “Niwape kitendawili, mkiweza kunipa jibu katika muda wa siku hizi saba za karamu, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Samsoni akawaambia, Mimi nitawategea ninyi kitendawili; kama mwaweza kunionyesha katika hizo siku saba za karamu, na kukitambua, ndipo hapo nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavao mengine thelathini;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Samsoni akawaambia, “Nitatega kitendawili. Kama mkiweza kutegua kitendawili hicho kwa muda wa siku saba za sherehe za harusi, basi, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi thelathini ya sikukuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Samsoni akawaambia, “Niwape kitendawili, mkiweza kunipa jibu katika muda wa siku hizi saba za karamu, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Samsoni akawaambia, “Niwape kitendawili, mkiweza kunipa jibu katika muda wa siku hizi saba za karamu, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Samsoni akawaambia, Mimi nitawategea ninyi kitendawili; kama mnaweza kunitegulia katika hizo siku saba za karamu, na kukitambua, ndipo nitakapowapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi thelathini ya sikukuu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Samsoni akawaambia, “Nitatega kitendawili. Kama mkiweza kutegua kitendawili hicho kwa muda wa siku saba za sherehe za harusi, basi, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi thelathini ya sikukuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Samusoni akawaambia: Na niwategee kitendawili! Kama mtaniambia maana yake siku hizi saba za karamu kwa kuitambua maana, basi, nitawapa ninyi kanzu 30 na mavazi mengine 30.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Samsoni akawaambia, Mimi nitawategea ninyi kitendawili; kama mwaweza kunionyesha katika hizo siku saba za karamu, na kukitambua, ndipo hapo nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavao mengine thelathini;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Samusoni akawaambia: “Nitatega kitendawili. Kama mukiweza kutegua kitendawili hicho kwa muda wa siku saba za sherehe za arusi, basi, nitawapa nguo makumi tatu za kitani na nguo makumi tatu za sikukuu.