Judges 14:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao wakamwambia, “Haya tega tusikie.” Samsoni akawaambia, “Kwa mla kukatoka mlo kwa mwenye nguvu, utamu.” Baada ya siku tatu hao vijana walikuwa bado hawajaweza kutegua hicho kitendawili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaambia, “Ndani ya mlaji, kulitoka kitu cha kuliwa, ndani ya mwenye nguvu, kulitoka kitu kitamu.” Kwa muda wa siku tatu hawakuweza kutoa jibu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akawaambia, Katika huyo mwenye kula kikatoka chakula, Katika huyo mwenye nguvu ukatoka utamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao wakamwambia, “Haya tega tusikie.” Samsoni akawaambia, “Kwa mla kukatoka mlo kwa mwenye nguvu, utamu.” Baada ya siku tatu hao vijana walikuwa bado hawajaweza kutegua hicho kitendawili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaambia, “Ndani ya mlaji, kulitoka kitu cha kuliwa, ndani ya mwenye nguvu, kulitoka kitu kitamu.” Kwa muda wa siku tatu hawakuweza kutoa jibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaambia, “Ndani ya mlaji, kulitoka kitu cha kuliwa, ndani ya mwenye nguvu, kulitoka kitu kitamu.” Kwa muda wa siku tatu hawakuweza kutoa jibu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akawaambia, Kutoka kwa huyo kikatoka chakula, Kutoka kwa huyo mwenye nguvu kikatoka kitamu. Nao katika siku tatu hawakuweza kukifumbua hicho kitendawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao wakamwambia, “Haya tega tusikie.” Samsoni akawaambia, “Kwa mla kukatoka mlo kwa mwenye nguvu, utamu.” Baada ya siku tatu hao vijana walikuwa bado hawajaweza kutegua hicho kitendawili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia: Kwa mlaji kikatoka chakula, kwa mwenye nguvu kikatoka kitamu. Siku tatu hawakuweza kumwambia maana ya hicho kitendawili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akawaambia, Katika huyo mwenye kula kikatoka chakula, Katika huyo mwenye nguvu ukatoka utamu. Nao katika siku tatu hawakuweza kukifungua hicho kitendawili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakamwambia: “Sasa tega tusikie.” Samusoni akawaambia: “Katika mwenye kula kukatoka chakula na katika mwenye nguvu kukatoka utamu.” Nyuma ya siku tatu hao vijana walikuwa bado hawajaweza kutegua hicho kitendawili.