Judges 14:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi siku ya saba wakamwambia mke wa Samsoni, “Mbembeleze mumeo ili atuambie maana ya kitendawili hicho, la sivyo tutakuteketeza kwa moto wewe pamoja na nyumba ya baba yako. Je, mlitualika hapa kuja kutunyanganya mali zetu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya nne, wakamwambia mkewe Samsoni, “Mbembeleze mumeo ili atutegulie hicho kitendawili, la sivyo tutakuchoma moto wewe na wa nyumba ya baba yako. Je, mmetualika ili mpate kutunyang’anya kile tulicho nacho?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa kwa siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, Mbembeleze mumeo, ili atuonyeshe hicho kitendawili, tusije tukakuteketeza moto wewe na nyumba ya baba yako; je! Mmetuita ili mpate kuichukua mali yetu? Je! Sivyo?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi siku ya saba wakamwambia mke wa Samsoni, “Mbembeleze mumeo ili atuambie maana ya kitendawili hicho, la sivyo tutakuteketeza kwa moto wewe pamoja na nyumba ya baba yako. Je, mlitualika hapa kuja kutunyang'anya mali zetu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, “Mbembeleze mumeo ili atueleze hicho kitendawili, la sivyo tutakuchoma moto wewe na wa nyumba ya baba yako. Je, mmetualika ili mpate kutunyang'anya kile tulicho nacho?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, “Mbembeleze mumeo ili atueleze hicho kitendawili, la sivyo tutakuchoma moto wewe na wa nyumba ya baba yako. Je, mmetualika ili mpate kutunyang’anya kile tulicho nacho?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa kwa siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, Mbembeleze mumeo, ili atutegulie hicho kitendawili, tusije tukakuteketeza moto wewe na nyumba ya baba yako; je! Mmetuita ili mpate kuichukua mali yetu? Je! Sivyo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi siku ya saba wakamwambia mke wa Samsoni, “Mbembeleze mumeo ili atuambie maana ya kitendawili hicho, la sivyo tutakuteketeza kwa moto wewe pamoja na nyumba ya baba yako. Je, mlitualika hapa kuja kutunyanganya mali zetu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa siku ya saba, wakamwambia mkewe Samusoni: Mnyege mumeo, atuambie hicho kitendawili, tusikuchome moto pamoja na nyumba ya baba yako! Je? Mmetualika kuja huku, mpate kuzichukua mali zetu! Au sivyo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa kwa siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, Mbembeleze mumeo, ili atuonyeshe hicho kitendawili, tusije tukakuteketeza moto wewe na nyumba ya baba yako; je! Mmetuita ili mpate kuichukua mali yetu? Je! Sivyo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi siku ya ine wakamwambia muke wa Samusoni: “Umubembeleze mume wako kusudi atuambie maana ya kitendawili hicho, kama sivyo tutakuteketeza kwa moto wewe pamoja na nyumba ya baba yako. Ninyi mulitualika hapa kutunyanganya mali zetu?”