Judges 14:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mke wa Samsoni akamwendea Samsoni, huku machozi yanamtiririka, akamwambia, “Kwa kweli unanichukia; hunipendi hata kidogo. Umewategea kitendawili watu wangu na hukuniambia maana yake.” Samsoni akamjibu, “Mimi sijawaeleza hata wazazi wangu. Sasa nitawezaje kukuambia wewe?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mke wa Samsoni akalia mbele yake na kumwambia, “Unanichukia! Hunipendi kabisa. Umewategea watu wangu kitendawili, lakini mimi hujaniambia jibu.” Samsoni akamwambia, “Tazama, sijamweleza baba yangu wala mama yangu, kwa nini nikufumbulie?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mkewe Samsoni akalia mbele yake, akasema, Wewe wanichukia tu, wala hunipendi; wewe umewategea kitendawili hao wana wa watu wangu, nawe hukuniambia mimi. Naye akamwambia, Angalia, sikumwambia baba yangu wala mama yangu, nami nikuambie wewe?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mke wa Samsoni akamwendea Samsoni, huku machozi yanamtiririka, akamwambia, “Kwa kweli unanichukia; hunipendi hata kidogo. Umewategea kitendawili watu wangu na hukuniambia maana yake.” Samsoni akamjibu, “Mimi sijawaeleza hata wazazi wangu. Sasa nitawezaje kukuambia wewe?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi mke wa Samsoni akalia mbele yake na kumwambia, “Unanichukia! Hunipendi kabisa. Umewategea watu wangu kitendawili, lakini mimi hujaniambia jibu.” Samsoni akamwambia, “Wala sijamweleza baba yangu wala mama yangu, kwa nini nikufumbulie?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi mke wa Samsoni akalia mbele yake na kumwambia, “Unanichukia! Hunipendi kabisa. Umewategea watu wangu kitendawili, lakini mimi hujaniambia jibu.” Samsoni akamwambia, “Wala sijamweleza baba yangu wala mama yangu, kwa nini nikufumbulie?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mkewe Samsoni akalia mbele yake, akasema, Wewe wanichukia tu, wala hunipendi; wewe umewategea kitendawili hao wana wa watu wangu, nawe hukuniambia mimi. Naye akamwambia, Angalia, sikumwambia baba yangu wala mama yangu, mbona nikuambie wewe?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mke wa Samsoni akamwendea Samsoni, huku machozi yanamtiririka, akamwambia, “Kwa kweli unanichukia; hunipendi hata kidogo. Umewategea kitendawili watu wangu na hukuniambia maana yake.” Samsoni akamjibu, “Mimi sijawaeleza hata wazazi wangu. Sasa nitawezaje kukuambia wewe?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mkewe Samusoni alipomlilia na kumwambia: Kumbe unachukizwa na mimi, hunipendi! Wana wao walio ukoo wangu umewategea kitendawili, lakini mimi hujaniambia. Akamwambia: Tazama, hata baba yangu na mama yangu sikuwaambia, wewe nitawezaje kukuambia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mkewe Samsoni akalia mbele yake, akasema, Wewe wanichukia tu, wala hunipendi; wewe umewategea kitendawili hao wana wa watu wangu, nawe hukuniambia mimi. Naye akamwambia, Angalia, sikumwambia baba yangu wala mama yangu, nami nikuambie wewe?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muke wa Samusoni akamwendea Samusoni, na machozi yakimutiririka, akamwambia: “Kwa kweli unanichukia; haunipendi hata kidogo. Umewategea kitendawili watu wangu na haukuniambia maana yake.” Samusoni akamujibu: “Mimi sijawaelezea hata wazazi wangu. Sasa nitaweza namna gani kukuelezea wewe?”