Judges 14:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini aliendelea kulia katika muda wao wote wa siku saba za sherehe za harusi. Siku ya saba Samsoni akamwambia mkewe kile kitendawili kwani alimbana sana. Mkewe akaenda haraka akawaambia watu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkewe akalia kwa muda wa zile siku zote saba za karamu. Hivyo siku ya saba Samsoni akamweleza, kwa kuwa aliendelea kumsisitiza sana. Naye mkewe akawaeleza watu wake kile kitendawili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akalia mbele yake hizo siku saba, wakati ulioendelea karamu yao; basi ikawa siku ya saba akamwambia, kwa sababu alikuwa akimsisitiza sana; naye akawaambia wale wana wa watu wake hicho kitendawili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini aliendelea kulia katika muda wao wote wa siku saba za sherehe za harusi. Siku ya saba Samsoni akamwambia mkewe kile kitendawili kwani alimbana sana. Mkewe akaenda haraka akawaambia watu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkewe akalia kwa muda wa zile siku zote saba za karamu. Hivyo siku ile ya saba Samsoni akamweleza, kwa kuwa aliendelea kumsisitiza sana. Naye akawaeleza watu wake kile kitendawili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkewe akalia kwa muda wa zile siku zote saba za karamu. Hivyo siku ile ya saba Samsoni akamweleza, kwa kuwa aliendelea kumsisitiza sana. Naye akawaeleza watu wake kile kitendawili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akalia mbele yake kwa hizo siku saba, za karamu yao; basi ikawa siku ya saba akamwambia, kwa sababu alikuwa akimsisitiza sana; naye akawaambia wale wana wa watu wake hicho kitendawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini aliendelea kulia katika muda wao wote wa siku saba za sherehe za harusi. Siku ya saba Samsoni akamwambia mkewe kile kitendawili kwani alimbana sana. Mkewe akaenda haraka akawaambia watu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipomlilia hizo siku saba za karamu yao, basi, siku ya saba akamwambia maana, kwani alimsumbua sana, naye akawaambia hicho kitendawili wale wana wa ukoo wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akalia mbele yake hizo siku saba, wakati ulioendelea karamu yao; basi ikawa siku ya saba akamwambia, kwa sababu alikuwa akimsisitiza sana; naye akawaambia wale wana wa watu wake hicho kitendawili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini aliendelea kulia katika muda wao wote wa siku saba za sherehe za arusi. Siku ya saba Samusoni akamwambia muke wake kile kitendawili kwa sababu alimwuzi sana. Muke wake akaenda haraka akawaambia watu wake.