Judges 14:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo ya saba, kabla ya jua kutua, wakamwambia Samsoni, “Ni kitu gani kitamu kuliko asali? Ni nani mwenye nguvu kuliko simba?” Samsoni akawajibu, “Kama hamngejishughulisha na mtamba wangu hamngeweza kukitegua kitendawili changu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya saba, kabla ya jua kutua, wanaume wa mji wakamwambia Samsoni, “Ni nini kilicho kitamu kuliko asali? Ni nini chenye nguvu kuliko simba?” Samsoni akawaambia, “Kama hamkulima na mtamba wangu, msingekitegua kitendawili changu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo ya saba, kabla ya jua kutua, wakamwambia Samsoni, “Ni kitu gani kitamu kuliko asali? Ni nani mwenye nguvu kuliko simba?” Samsoni akawajibu, “Kama hamngejishughulisha na mtamba wangu hamngeweza kukitegua kitendawili changu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya saba kabla ya jua kutua, watu wa mji wakamwambia Samsoni, “Ni nini kitamu kama asali? Ni nini chenye nguvu kama simba?” Samsoni akawaambia, “Kama hamkulima na mtamba wangu, hamngeweza kufumbua kitendawili changu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya saba kabla ya jua kutua, watu wa mji wakamwambia Samsoni, “Ni nini kitamu kama asali? Ni nini chenye nguvu kama simba?” Samsoni akawaambia, “Kama hamkulima na mtamba wangu, hamngeweza kufumbua kitendawili changu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa, Ni kitu gani kilicho kitamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu kuliko simba? Naye akawaambia, Msingelima na mtamba wangu, Hamngekitegua kitendawili changu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo ya saba, kabla ya jua kutua, wakamwambia Samsoni, “Ni kitu gani kitamu kuliko asali? Ni nani mwenye nguvu kuliko simba?” Samsoni akawajibu, “Kama hamngejishughulisha na mtamba wangu hamngeweza kukitegua kitendawili changu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo watu wa ule mji wakamwambia siku ya saba, jua lilipokuwa halijachwa bado: Kiko kitamu kuliko asali? Yuko mwenye nguvu kuliko simba? Naye akawaambia: Kama hamngalimtumia ndama wangu, hapo mlipolima, hicho kitendawili changu hamngaliona maana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa, Ni kitu gani kilicho tamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu kuliko simba? Naye akawaambia, Kwamba hamkulima na mtamba wangu, Hamngekitambua kitendawili changu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo ya saba, mbele ya jua kutua, wakamwambia Samusoni, “Ni kitu gani kitamu kuliko asali? Ni nani mwenye nguvu kuliko simba?” Samusoni akawajibu: “Kama hamungejishugulisha na mwana-ngombe wangu hamungeweza kukitegua kitendawili changu.”