Judges 14:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu, naye akaenda mjini Ashkeloni, akawaua watu thelathini, kisha akachukua mavazi yao ya sikukuu, akawapa wale waliotegua kitendawili chake. Halafu akaondoka, akaenda nyumbani kwa wazazi wake akiwa na hasira kali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Roho wa Mwenyezi Mungu akamjia Samsoni kwa nguvu. Samsoni akateremka hadi Ashkeloni, akawaua wanaume thelathini wa mji huo, akatwaa mali yao, akawapa watu wale waliotegua kile kitendawili nguo zao. Akiwa amejaa hasira, akakwea kurudi nyumbani kwa baba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Roho ya Bwana ikamjilia juu yake kwa nguvu, naye akatelemkia Ashkeloni, akapiga watu waume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili mavao hayo. Hasira zake zikamwaka, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu, naye akaenda mjini Ashkeloni, akawaua watu thelathini, kisha akachukua mavazi yao ya sikukuu, akawapa wale waliotegua kitendawili chake. Halafu akaondoka, akaenda nyumbani kwa wazazi wake akiwa na hasira kali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Roho wa BWANA akamjia Samsoni kwa nguvu. Akatelemka mpaka Ashkeloni, akawaua watu waume thelathini miongoni mwa watu wa mji, akatwaa mali zao na nguo zao, akawapa watu wale waliofumbua kile kitendawili. Akiwa na hasira, akakwea kurudi nyumbani kwa baba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Roho wa bwana akamjia Samsoni kwa nguvu. Akateremka mpaka Ashkeloni, akawaua watu waume thelathini miongoni mwa watu wa mji, akatwaa mali zao na nguo zao, akawapa watu wale waliofumbua kile kitendawili. Akiwa na hasira, akakwea kurudi nyumbani kwa baba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Roho ya BWANA ikamjia juu yake kwa nguvu, naye akateremka hadi Ashkeloni, akawaua wanaume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili mavazi hayo ya sikukuu. Hasira zake zikampanda, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu, naye akaenda mjini Ashkeloni, akawaua watu thelathini, kisha akachukua mavazi yao ya sikukuu, akawapa wale waliotegua kitendawili chake. Halafu akaondoka, akaenda nyumbani kwa wazazi wake akiwa na hasira kali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu, akatelemka kwenda Askaloni, akaua huko watu 30, akachukua yote, waliyokuwa nayo, nayo mavazi akawapa wao waliomwambia maana ya kitendawili, lakini makali yake yakawaka moto, aliporudi nyumbani mwa baba yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Roho ya BWANA ikamjilia juu yake kwa nguvu, naye akatelemkia Ashkeloni, akapiga watu waume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili mavao hayo. Hasira zake zikamwaka, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo roho wa Yawe akamushika Samusoni kwa nguvu, naye akaenda muji Askeloni, akawaua watu makumi tatu, kisha akatwaa nguo zao za sikukuu, akawapa wale waliotegua kitendawili chake. Halafu akaondoka, akaenda kwa nyumba kwa wazazi wake akiwa na hasira kali.