Judges 14:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliporudi nyumbani akawaambia wazazi wake, “Nimemwona msichana mmoja Mfilisti huko Timna. Niozeni msichana huyo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipopanda kutoka huko, akawaambia baba yake na mama yake, “Nimemwona mwanamke Mfilisti huko Timna; basi mnitwalie awe mke wangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliporudi nyumbani akawaambia wazazi wake, “Nimemwona msichana mmoja Mfilisti huko Timna. Niozeni msichana huyo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipopanda kutoka huko, akawaambia baba yake na mama yake, “Nimemwona mwanamke wa Kifilisti huko Timna; basi mnipatie ili awe mke wangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipopanda kutoka huko, akawaambia baba yake na mama yake, “Nimemwona mwanamke wa Kifilisti huko Timna; basi mnipe ili awe mke wangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemuona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa mabinti za Wafilisti; basi mniruhusu, nimuoe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliporudi nyumbani akawaambia wazazi wake, “Nimemwona msichana mmoja Mfilisti huko Timna. Niozeni msichana huyo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipopanda kwao akamwambia baba yake na mama yake kwamba: Nimeona mwanamke huko Timuna kwao vijana wa kike wa Wafilisti, sasa mchukueni, awe mke wangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliporudi kwa nyumba akawaambia wazazi wake: “Nimemwona binti mumoja Mufilistini kule Timuna. Munioee binti huyo.”