Judges 14:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wazazi wake wakamwambia, “Je, hakuna msichana yeyote miongoni mwa ndugu zako au kati ya watu wetu hata uende kuoa kwa Wafilisti wasiotahiriwa?” Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Niozeni msichana huyo, maana ananipendeza sana.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baba yake na mama yake wakamjibu, “Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa watu wetu wote, hata ulazimike kwenda kujitwalia mke kutoka kwa hao Wafilisti wasiotahiriwa?” Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Nipatieni huyo kwa maana ndiye alinipendeza.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wazazi wake wakamwambia, “Je, hakuna msichana yeyote miongoni mwa ndugu zako au kati ya watu wetu hata uende kuoa kwa Wafilisti wasiotahiriwa?” Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Niozeni msichana huyo, maana ananipendeza sana.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baba yake na mama yake wakamjibu, “Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa ndugu zako, hata ulazimike kwenda kujitwalia mwanamke kutoka kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa?” Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Nipatieni huyo kwa maana ndiye aliyenipendeza.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baba yake na mama yake wakamjibu, “Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa ndugu zako, hata ulazimike kwenda kujitwalia mwanamke kutoka kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa?” Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Nipatieni huyo kwa maana ndiye alinipendeza.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu wote, hata uende kumuoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mniruhusu nimuoe huyo, kwa maana ananipendeza sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wazazi wake wakamwambia, “Je, hakuna msichana yeyote miongoni mwa ndugu zako au kati ya watu wetu hata uende kuoa kwa Wafilisti wasiotahiriwa?” Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Niozeni msichana huyo, maana ananipendeza sana.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baba yake na mama yake wakamwambia: Kumbe kwetu hakuna mwanamke kwao vijana wa kike wa ndugu zako walio ukoo wetu, wewe ukienda kuchukua mwanamke kwao Wafilisti wasiotahiriwa? Lakini Samusoni akamwambia baba yake: Huyo mchukue, awe mke wangu! Kwani ndiye apendezaye machoni pangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wazazi wake wakamwambia: “Hakuna binti yeyote kati ya wandugu zako au kati ya watu wetu kusudi uende kuoa kwa Wafilistini wasiotahiriwa?” Lakini Samusoni akamwambia baba yake: “Munioee binti huyo, maana ananipendeza sana.”