Judges 14:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Samsoni na wazazi wake waliondoka kwenda Timna. Walipofika huko kwenye mashamba ya mizabibu, mwanasimba mmoja akatokea akamngurumia Samsoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Samsoni akateremka Timna pamoja na baba yake na mama yake. Walipofika kwenye mashamba ya mizabibu huko Timna, ghafula mwana simba akamjia akimngurumia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Samsoni na wazazi wake waliondoka kwenda Timna. Walipofika huko kwenye mashamba ya mizabibu, mwanasimba mmoja akatokea akamngurumia Samsoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Samsoni akatelemkia Timna pamoja na baba yake na mama yake. Walipofika kwenye mashamba ya mizabibu huko Timna, ghafula mwana simba akamjia akimngurumia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Samsoni akateremkia Timna pamoja na baba yake na mama yake. Walipofika kwenye mashamba ya mizabibu huko Timna, ghafula mwana simba akamjia akimngurumia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakateremka hadi Timna, walipofika katika mashamba ya mizabibu huko Timna; mara, mwanasimba akamngurumia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Samsoni na wazazi wake waliondoka kwenda Timna. Walipofika huko kwenye mashamba ya mizabibu, mwanasimba mmoja akatokea akamngurumia Samsoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Samusoni alipotelemka kwenda Timuna pamoja na baba yake na mama yake, hapo, walipofika kwenye mizabibu ya Timuna, mara mwana wa simba akamkingia njiani na kumngurumia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Samusoni na wazazi wake wakaondoka kwenda Timuna. Walipofika kule kwenye mashamba ya mizabibu, simba mukali mumoja akatokea akamungurumia Samusoni.