Judges 14:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya siku chache alirudi huko Timna kumchukua huyo msichana. Alipokuwa njiani akageuka pembeni kuuona mzoga wa yule simba, na kumbe kulikuwa na nyuki ndani ya mzoga na asali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya muda, Samsoni aliporudi ili akamwoe, akageuka kando ili kuutazama mzoga wa yule simba. Tazama! Ndani ya ule mzoga akaona kundi la nyuki na asali kiasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha baadaye akarudi ili kumtwaa, naye akageuka kando kuuangalia mzoga wa huyo simba; na tazama, nyuki wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na asali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya siku chache alirudi huko Timna kumchukua huyo msichana. Alipokuwa njiani akageuka pembeni kuuona mzoga wa yule simba, na kumbe kulikuwa na nyuki ndani ya mzoga na asali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya muda aliporudi ili akamwoe, akatazama kando ili kuutazama mzoga wa yule simba, na tazama, kulikuwa na kundi la nyuki ndani ya ule mzoga wa simba na kulikuwa na asali;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya muda aliporudi ili akamwoe, akatazama kando ili kuutazama mzoga wa yule simba, na tazama, kulikuwa na kundi la nyuki ndani ya ule mzoga wa simba na kulikuwa na asali;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha baadaye akarudi ili kumtwaa, naye akaenda kando kuuangalia mzoga wa huyo simba; na tazama, nyuki wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na asali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya siku chache alirudi huko Timna kumchukua huyo msichana. Alipokuwa njiani akageuka pembeni kuuona mzoga wa yule simba, na kumbe kulikuwa na nyuki ndani ya mzoga na asali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zilipopita, akarudi kumchukua. Alipotoka njiani, aende kuutazama ule mzoga wa yule simba, akaona, nyuki wengi wa porini wamo ndani ya mzoga wa simba, hata asali imo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha baadaye akarudi ili kumtwaa, naye akageuka kando kuuangalia mzoga wa huyo simba; na tazama, nyuki wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na asali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya siku chache akarudi kule Timuna kwa kumutwaa yule binti. Alipokuwa katika njia akageuka pembeni kwa kuangalia muzoga wa yule simba, kumbe kulikuwa nyuki na asali ndani ya muzoga.