Judges 14:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akapakua asali kwa mikono yake akawa anakula huku akiendelea na safari yake. Aliporudi kwa wazazi wake, akawapa asali kidogo nao wakala. Lakini hakuwaambia kwamba alitoa asali hiyo ndani ya mzoga wa simba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akachukua asali mkononi mwake, akala huku akitembea. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa kiasi cha ile asali, nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa aliitwaa asali katika mzoga wa simba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akatwaa asali mikononi mwake akaenda mbele, huku akila alipokuwa akienenda, akawafikilia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akapakua asali kwa mikono yake akawa anakula huku akiendelea na safari yake. Aliporudi kwa wazazi wake, akawapa asali kidogo nao wakala. Lakini hakuwaambia kwamba alitoa asali hiyo ndani ya mzoga wa simba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akachukua asali mkononi mwake akaendelea huku akila. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa ile asali nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa alitwaa asali kutoka kwenye mzoga wa simba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akachukua asali mkononi mwake akaendelea huku akila. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa ile asali nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa alitwaa asali kutoka kwenye mzoga wa simba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akatwaa asali mikononi mwake akasonga mbele, huku akila alipokuwa akienda, akawafikia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akapakua asali kwa mikono yake akawa anakula huku akiendelea na safari yake. Aliporudi kwa wazazi wake, akawapa asali kidogo nao wakala. Lakini hakuwaambia kwamba alitoa asali hiyo ndani ya mzoga wa simba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaitwaa mikononi mwake, akaendelea njiani akiila. Kisha akaenda kwao baba yake na mama yake, akawapa nao, nao wakaila, lakini hakuwaambia, ya kuwa asali hii ameitwaa katika mzoga wa simba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akatwaa asali mikononi mwake akaenda mbele, huku akila alipokuwa akienenda, akawafikilia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, akapakua asali kwa mikono yake, akaikula akiendelea na safari yake. Aliporudi kwa wazazi wake, akawapa asali kidogo nao wakakula. Lakini hakuwaambia kwamba alitosha asali hiyo ndani ya muzoga wa simba.