Judges 15:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipofika Lehi, Wafilisti walimwendea mbio huku wakipiga kelele. Ghafla roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu na zile kamba walizomfunga mikononi mwake zikakatika kama kitani kilichoshika moto, navyo vifungo vikaanguka chini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipofika Lehi, Wafilisti walimwendea mbio huku wakipiga kelele. Ghafla roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu na zile kamba walizomfunga mikononi mwake zikakatika kama kitani kilichoshika moto, navyo vifungo vikaanguka chini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa BWANA akamjia juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono yake zikawa kama katani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa bwana akamjia juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono yake zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipofika Lehi, Wafilisti walimwendea mbio huku wakipiga kelele. Ghafla roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu na zile kamba walizomfunga mikononi mwake zikakatika kama kitani kilichoshika moto, navyo vifungo vikaanguka chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeye alipofika Lehi, Wafilisti wakamawendea njiani na kumzomea. Ndipo, roho ya Bwana ilipomjia kwa nguvu, nazo kamba, ambazo mikono ilifungwa nazo, zikawa kama nyuzi zilizounguzwa na moto, pingu zake nazo zikayeyuka na kuanguka mikononi pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipofika Lehi, Wafilistini wakamwendea mbio na walikuwa wanapiga kelele. Kwa rafla roho wa Yawe akamushika Samusoni kwa nguvu na zile kamba walizomufunga kwenye mikono yake zikakatika kama kitani kilichoguswa na moto, navyo vifungo vikaanguka chini.