Judges 15:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu akafungua mahali palipokuwa na shimo huko Leki, akatiririsha maji. Samsoni akanywa maji hayo na nguvu zake zikamrudia. Chemchemi hiyo ikaitwa En-hakore; nayo iko huko Lehi mpaka leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mungu akafunua shimo huko Lehi, na maji yakatoka. Samsoni alipoyanywa maji hayo, nguvu zikamrudia, akahuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore, nayo iko hadi leo huko Lehi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokwisha kunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu akafungua mahali palipokuwa na shimo huko Leki, akatiririsha maji. Samsoni akanywa maji hayo na nguvu zake zikamrudia. Chemchemi hiyo ikaitwa En-hakore; nayo iko huko Lehi mpaka leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akafunua shimo huko Lehi, pakatoka maji. Samsoni alipoyanywa, nguvu zikamrudia na kuhuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore, nayo iko mpaka leo huko Lehi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akafunua shimo huko Lehi, pakatoka maji. Samsoni alipoyanywa, nguvu zikamrudia na kuhuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore, nayo iko mpaka leo huko Lehi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore, napo papo katika Lehi hata hivi leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu akafungua mahali palipokuwa na shimo huko Leki, akatiririsha maji. Samsoni akanywa maji hayo na nguvu zake zikamrudia. Chemchemi hiyo ikaitwa En-hakore; nayo iko huko Lehi mpaka leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Mungu alipopasua shimo lililoko Lehi, mara yakatoka maji humo, naye akanywa, mpaka roho yake ikamrudia, akapata kuwa mzima tena. Kwa hiyo hapo huitwa Chemchemi ya Mliaji, nayo iko huko Lehi hata siku hii ya leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokwisha kunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore, napo pa katika Lehi hata hivi leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu akafungua pahali palipokuwa shimo kule Lehi, akatiririsha maji. Samusoni akakunywa maji hayo na nguvu zake zikamurudilia. Chemichemi hiyo ikaitwa “Kisima cha Yule Anayeita” nayo iko kule Lehi mpaka leo.