Judges 16:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati Samsoni alipokuwa analala Delila akavisuka pamoja vishungi saba vya nywele za Samsoni akavifunga kwa mtandio wa nguo na kuvikaza kabisa kwa kigingi. Kisha akamwambia Samsoni, “Samsoni! Wafilisti wanakuja kukushambulia.” Samsoni akaamka kutoka usingizini akakingoa kile kigingi na kuutatua ule mtandio wa nguo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na kuukaza kwa msumari. Kisha akamwambia, “Samsoni, Wafilisti wanakujia!” Samsoni akaamka kutoka usingizini na kung’oa msumari na mtande, pamoja na ile nguo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung'oa ule msumari, na ule mtande.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati Samsoni alipokuwa analala Delila akavisuka pamoja vishungi saba vya nywele za Samsoni akavifunga kwa mtandio wa nguo na kuvikaza kabisa kwa kigingi. Kisha akamwambia Samsoni, “Samsoni! Wafilisti wanakuja kukushambulia.” Samsoni akaamka kutoka usingizini akaking'oa kile kigingi na kuutatua ule mtandio wa nguo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na kuvikaza kwa msumari. Kisha akamwambia, “Samsoni, Wafilisti wanakujia!” Lakini akaamka kutoka usingizini na kuung'oa ule msumari na ule mtande.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na kuvikaza kwa msumari. Kisha akamwambia, “Samsoni, Wafilisti wanakujia!” Lakini akaamka kutoka usingizini na kuung’oa ule msumari na ule mtande.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung'oa ule msumari, na ule mtande.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati Samsoni alipokuwa analala Delila akavisuka pamoja vishungi saba vya nywele za Samsoni akavifunga kwa mtandio wa nguo na kuvikaza kabisa kwa kigingi. Kisha akamwambia Samsoni, “Samsoni! Wafilisti wanakuja kukushambulia.” Samsoni akaamka kutoka usingizini akakingoa kile kigingi na kuutatua ule mtandio wa nguo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwisha kuzipigilia kwa uwambo akamwambia: Wafilisti wanakujia, Samusoni; ndipo, alipoamka katika usingizi, akaung'oa ule uwambo wa kufumia pamoja na nyuzi za mtande.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung’oa ule msumari, na ule mtande.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Samusoni alipokuwa analala Delila akasuka nywele za Samusoni kwa misuko saba na nyuzi, akazifunga kwa chombo cha kufuma nguo na kukaza kabisa kwenye musumari. Kisha akamwambia Samusoni: “Samusoni! Wafilistini wanakuja kukushambulia.” Samusoni akaamuka kutoka katika usingizi akauongoa ule musumari na kutatua kile chombo cha kufuma nguo.