Judges 16:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Delila alipoona kwamba Samsoni amemwambia siri yake yote, akawaita wakuu wa Wafilisti, akawaambia, “Njoni safari hii moja tu maana Samsoni ameniambia siri yake yote.” Wakuu wa Wafilisti wakamwendea Delila huku wamemletea fedha walizomwahidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Delila alipoona kuwa amemweleza siri yake yote, akatuma ujumbe kwa viongozi wa Wafilisti na kusema, “Njooni tena mara nyingine, maana amenieleza siri yake yote.” Basi viongozi wa Wafilisti wakarudi kwa Delila, wakiwa na fedha mikononi mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Delila alipoona kwamba Samsoni amemwambia siri yake yote, akawaita wakuu wa Wafilisti, akawaambia, “Njoni safari hii moja tu maana Samsoni ameniambia siri yake yote.” Wakuu wa Wafilisti wakamwendea Delila huku wamemletea fedha walizomwahidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Delila alipoona kuwa amemweleza siri yake yote, akatuma ujumbe kwa viongozi wa Wafilisti na kusema, “Njoni tena mara nyingine, maana amenieleza siri yake yote.” Basi viongozi wa Wafilisti wakaja kwa Delila, wakiwa na fedha mikononi mwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Delila alipoona kuwa amemweleza siri yake yote, akatuma ujumbe kwa viongozi wa Wafilisti na kusema, “Njooni tena mara nyingine, maana amenieleza siri yake yote.” Basi viongozi wa Wafilisti wakaja kwa Delila, wakiwa na fedha mikononi mwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia siri yake yote. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Delila alipoona kwamba Samsoni amemwambia siri yake yote, akawaita wakuu wa Wafilisti, akawaambia, “Njoni safari hii moja tu maana Samsoni ameniambia siri yake yote.” Wakuu wa Wafilisti wakamwendea Delila huku wamemletea fedha walizomwahidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Delila alipoona, ya kuwa amemjulisha yote yaliyokuwamo moyoni mwake, akatuma kuwaita watu wa Wafilisti kwamba: Pandeni mara hii tu! Kwani amenijulisha yote yaliyokuwamo moyoni mwake. Nao wakuu wa Wafilisti walipopanda kufika kwake walishika zile fedha mikononi mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Delila alipoona kwamba Samusoni amemwambia siri yake yote, akawaita wakubwa wa Wafilistini, akawaambia: “Mukuje mara hii moja tu maana Samusoni ameniambia siri yake yote.” Wakubwa wa Wafilistini wakamwendea Delila na walikuwa wanamuletea feza walizomwahidi.