Judges 16:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Gaza walipoambiwa kuwa Samsoni yuko huko, walilizingira eneo hilo na kumvizia kwenye lango la mji usiku kucha. Wakakaa kimya huko langoni usiku wote wakifikiri kwamba wanaweza kungojea mpaka mapambazuko wapate kumuua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa Gaza wakaambiwa, “Samsoni amekuja huku!” Hivyo, wakapazingira mahali pale, nao wakamvizia usiku kucha penye lango la mji. Wakakaa kimya usiku kucha, wakiwaza, “Kutakapopambazuka, tutamuua.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Gaza walipoambiwa kuwa Samsoni yuko huko, walilizingira eneo hilo na kumvizia kwenye lango la mji usiku kucha. Wakakaa kimya huko langoni usiku wote wakifikiri kwamba wanaweza kungojea mpaka mapambazuko wapate kumuua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa Gaza wakaambiwa, “Samsoni amekuja huku!” Hivyo wakapazingira pale mahali nao wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji. Wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, “Tumvizie hadi mapambazuko, ndipo tutamwua.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa Gaza wakaambiwa, “Samsoni amekuja huku!” Hivyo wakapazingira mahali pale nao wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji. Wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, “Tumvizie hadi mapambazuko, ndipo tutamuua.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Gaza walipoambiwa kuwa Samsoni yuko huko, walilizingira eneo hilo na kumvizia kwenye lango la mji usiku kucha. Wakakaa kimya huko langoni usiku wote wakifikiri kwamba wanaweza kungojea mpaka mapambazuko wapate kumuua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wagaza walipoambiwa, ya kuwa Samusoni ameingia humo, wakaizunguka hiyo nyumba na kumvizia usiku wote penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha kwa kwamba: Tungoje mapambazuko ya asubuhi, tupate kumwua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Gaza walipoambiwa kwamba Samusoni yuko kule, wakalizunguka eneo hilo na kumuvizia kwenye mulango wa muji usiku kucha. Wakakaa kimya kule kwenye mulango usiku wote wakifikiri kwamba wanaweza kungojea mpaka mapambazuko wapate kumwua.