Judges 16:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Delila akamwambia Samsoni, “Samsoni! Wafilisti wanakuja kukushambulia!” Samsoni akaamka usingizini huku akifikiri kwamba atatoka na kujiokoa kama hapo awali. Kumbe hakujua kwamba Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwacha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mwanamke akamwita, “Samsoni! Hao, Wafilisti wanakujia!” Akaamka toka usingizini, akisema, “Nitatoka nje kama hapo awali; nitajinyoosha, niwe huru.” Lakini hakujua kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amemwacha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa Bwana amemwacha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Delila akamwambia Samsoni, “Samsoni! Wafilisti wanakuja kukushambulia!” Samsoni akaamka usingizini huku akifikiri kwamba atatoka na kujiokoa kama hapo awali. Kumbe hakujua kwamba Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwacha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mwanamke akamwita, “Samsoni, hao Wafilisti wanakujia!” Akaamka toka usingizini akasema, “Nitatoka nje kama hapo awali, nitawakung'utia mbali na kuwa huru.” Lakini hakujua kuwa BWANA amemwacha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mwanamke akamwita, “Samsoni, hao Wafilisti wanakujia!” Akaamka toka usingizini akasema, “Nitatoka nje kama hapo awali, nitawakung’utia mbali na kuwa huru.” Lakini hakujua kuwa bwana amemwacha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Delila akamwambia Samsoni, “Samsoni! Wafilisti wanakuja kukushambulia!” Samsoni akaamka usingizini huku akifikiri kwamba atatoka na kujiokoa kama hapo awali. Kumbe hakujua kwamba Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwacha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akasema: Wafilisti wanakujia, Samusoni. Alipoamka katika usingizi, alisema moyoni: Nitatoka kama mara nyingine zote kwa kujinyosha tu, kwani hakujua, ya kuwa Bwana ameondoka kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Delila akamwambia Samusoni: “Samusoni! Wafilistini wanakuja kukushambulia!” Samusoni akaamuka toka katika usingizi naye akifikiri kwamba atatoka na kujiokoa kama vile mbele. Kumbe hakujua kwamba Yawe alikuwa amemwacha.