Judges 16:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafilisti walimkamata, wakamngoa macho, wakampeleka Gaza, wakamfunga kwa pingu za shaba, na kumlazimisha kufanya kazi ya kusaga unga huko gerezani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho yake, wakamteremsha hadi Gaza. Wakamfunga kwa pingu za shaba, wakamweka gerezani ili asage ngano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafilisti walimkamata, wakamng'oa macho, wakampeleka Gaza, wakamfunga kwa pingu za shaba, na kumlazimisha kufanya kazi ya kusaga unga huko gerezani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho yake wakamchukuwa wakamtelemsha mpaka Gaza. Wakiwa wamemfunga kwa pingu za shaba, wakamweka ili asage ngano huko gerezani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho yake, wakamchukua wakamteremsha mpaka Gaza. Wakiwa wamemfunga kwa pingu za shaba, wakamweka ili asage ngano huko gerezani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafilisti walimkamata, wakamngoa macho, wakampeleka Gaza, wakamfunga kwa pingu za shaba, na kumlazimisha kufanya kazi ya kusaga unga huko gerezani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Wafilisti walipomkamata, wakamchoma macho, wakamshusha kumpeleka Gaza, wakamfunga kwa minyororo miwili ya shaba, kisha akawa kifungoni akisaga unga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafilistini wakamukamata, wakamwongoa macho, wakamupeleka Gaza, wakamufunga kwa minyororo ya shaba, na kumulazimisha kufanya kazi ya kusaga unga kule katika kifungo.