Judges 16:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakuu wa Wafilisti walikusanyika ili kusherehekea na kumtolea tambiko mungu wao aitwaye Dagoni. Basi, wakawa wanaimba, “Mungu wetu amemtia mikononi mwetu adui yetu Samsoni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi viongozi wa Wafilisti wakakusanyika pamoja ili kutoa kafara kuu kwa mungu wao Dagoni, wakisherehekea na kusema, “Mungu wetu amemtia adui yetu Samsoni mikononi mwetu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakuu wa Wafilisti walikusanyika ili kusherehekea na kumtolea tambiko mungu wao aitwaye Dagoni. Basi, wakawa wanaimba, “Mungu wetu amemtia mikononi mwetu adui yetu Samsoni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi viongozi wa Wafilisti wakakusanyika pamoja ili kutoa kafara kwa mungu wao Dagoni na kufanya karamu, wakisema, “Mungu wetu amemtia adui yetu Samsoni mikononi mwetu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi viongozi wa Wafilisti wakakusanyika pamoja ili kutoa kafara kwa mungu wao Dagoni na kufanya karamu, wakisema, “Mungu wetu amemtia adui yetu Samsoni mikononi mwetu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, mungu wetu amemtia Samsoni adui yetu mikononi mwetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakuu wa Wafilisti walikusanyika ili kusherehekea na kumtolea tambiko mungu wao aitwaye Dagoni. Basi, wakawa wanaimba, “Mungu wetu amemtia mikononi mwetu adui yetu Samsoni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wa Wafilisti walipokusanyika kufanya sikukuu ya tambiko kubwa ya mungu wao Dagoni wakamfurahia kwamba: Mungu wetu ametupa adui yetu Samusoni mikononi mwetu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wa Wafilistini wakakusanyika kwa kusherehekea na kumutolea mungu wao anayeitwa Dagoni sadaka. Basi, wakakuwa wanaimba: “Mungu wetu amemutia adui yetu Samusoni katika mikono yetu.”