Judges 16:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipojawa na furaha sana mioyoni mwao, wakasema, “Mleteni Samsoni atutumbuize.” Basi wakamtoa Samsoni gerezani, wakamleta naye akawatumbuiza. Wakamweka katikati ya nguzo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mioyo yao ilipokuwa imefurahishwa, wakapaza sauti, wakisema, “Mleteni Samsoni aje ili atutumbuize.” Basi wakamleta Samsoni kutoka gerezani, naye akawatumbuiza. Wakamsimamisha katikati ya nguzo mbili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipojawa na furaha sana mioyoni mwao, wakasema, “Mleteni Samsoni atutumbuize.” Basi wakamtoa Samsoni gerezani, wakamleta naye akawatumbuiza. Wakamweka katikati ya nguzo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mioyo yao ilipokuwa imefurahishwa wakasema, “Mleteni Samsoni aje acheze ili tufurahi.” Basi wakamleta Samsoni kutoka mle gerezani naye akacheza mbele yao. Wakamweka kati ya nguzo mbili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mioyo yao ilipokuwa imefurahishwa wakasema, “Mleteni Samsoni aje acheze ili tufurahi.” Basi wakamleta Samsoni kutoka mle gerezani naye akacheza mbele yao. Wakamweka kati ya nguzo mbili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipojawa na furaha sana mioyoni mwao, wakasema, “Mleteni Samsoni atutumbuize.” Basi wakamtoa Samsoni gerezani, wakamleta naye akawatumbuiza. Wakamweka katikati ya nguzo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mioyo yao ilipochangamka, wakasema: Mwiteni Samusoni, atuchezee! Wakamwita Samusoni na kumtoa kifungoni, awachezee. Walipomsimamisha katikati ya nguzo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipojaa na furaha sana ndani ya mioyo yao, wakasema: “Mulete Samusoni atuchekeshe.” Basi wakamutosha Samusoni katika kifungo, wakamuleta naye akawachekesha. Wakamuweka katikati ya nguzo.