Judges 16:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jumba hilo lilikuwa limejaa watu: Wakuu wote wa Wafilisti walikuwapo na kwenye paa kulikuwa na watu 3,000 wanaume na wanawake, wakimtazama Samsoni akiwatumbuiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi lile jengo lilikuwa na wanaume na wanawake wengi; viongozi wote wa Wafilisti walikuwa humo, na kwenye dari walikuwepo watu wapatao elfu tatu, wanaume kwa wanawake, wakimtazama Samsoni akiwatumbuiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jumba hilo lilikuwa limejaa watu: wakuu wote wa Wafilisti walikuwapo na kwenye paa kulikuwa na watu 3,000 wanaume na wanawake, wakimtazama Samsoni akiwatumbuiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi lile jengo lilikuwa na wingi wa watu waume kwa wake; viongozi wote wa Wafilisti walikuwemo humo, na kwenye sakafu ya juu walikuwepo watu 3,000 waume kwa wake, waliokuwa wakimtazama Samsoni wakati anacheza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi lile jengo lilikuwa na wingi wa watu waume kwa wake; viongozi wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na kwenye sakafu ya juu walikuwepo watu 3,000 waume kwa wake, waliokuwa wakimtazama Samsoni wakati anacheza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi nyumba ile ilikuwa imejaa wanaume kwa wanawake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu wanaume kwa wanawake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jumba hilo lilikuwa limejaa watu: Wakuu wote wa Wafilisti walikuwapo na kwenye paa kulikuwa na watu 3,000 wanaume na wanawake, wakimtazama Samsoni akiwatumbuiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo hiyo nyumba ilikuwa imejaa watu waume na wake, nao wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo, namo darini walikuwamo kama 3000 waume na wake, waliomtazama Samusoni, jinsi alivyocheza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyumba hiyo ilikuwa imejaa watu: wakubwa wote wa Wafilistini walikuwa mule na kwenye paa kulikuwa watu elfu tatu wanaume na wanawake, wakimutazama Samusoni akiwachekesha.