Judges 16:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Samsoni akamwomba Mwenyezi-Mungu: “Bwana Mwenyezi-Mungu nakuomba unikumbuke. Nitie nguvu, mara hii moja tu, ee Mungu, ili niwalipize kisasi mara moja hii tu Wafilisti ambao waliyangoa macho yangu mawili.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Samsoni akamwomba Mwenyezi Mungu, akasema, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi, unikumbuke. Ee Mungu, nakusihi ukanitie nguvu mara hii moja tu, ili kwa tendo hili nipate kulipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa sababu ya macho yangu mawili.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Samsoni akamwomba Mwenyezi-Mungu: “Bwana Mwenyezi-Mungu nakuomba unikumbuke. Nitie nguvu, mara hii moja tu, ee Mungu, ili niwalipize kisasi mara moja hii tu Wafilisti ambao waliyang'oa macho yangu mawili.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Samsoni akamwomba BWANA, akasema, “Ee BWANA Mwenyezi, unikumbuke. Ee Mungu, nakusihi ukanitie nguvu mara hii moja tena, ili kwa tendo hili nipate kulipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Samsoni akamwomba bwana, akasema, “Ee bwana Mwenyezi, unikumbuke. Ee Mungu, nakusihi ukanitie nguvu mara hii moja tena, ili kwa tendo hili nipate kulipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, nikumbuke nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Samsoni akamwomba Mwenyezi-Mungu: “Bwana Mwenyezi-Mungu nakuomba unikumbuke. Nitie nguvu, mara hii moja tu, ee Mungu, ili niwalipize kisasi mara moja hii tu Wafilisti ambao waliyangoa macho yangu mawili.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Samusoni alipomlilia Bwana kwamba: Bwana Mungu, nikumbuke, unitie nguvu hii mara moja tu, Mungu wangu, niwalipishe hawa Wafilisti kwa mara moja macho yangu mawili!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo Samusoni akamwomba Yawe: “Bwana wangu Yawe, ninakuomba unikumbuke. Unitie nguvu, mara hii moja tu, ee Mungu, kusudi niwalipize kisasi mara moja hii tu Wafilistini ambao waliyaongoa macho yangu mawili.”