Judges 16:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Samsoni akabaki mjini mpaka usiku wa manane. Wakati wa usiku wa manane akaamka akashika miimo miwili ya malango, akaingoa pamoja na makomeo yake akaibeba na kwenda nayo mpaka karibu na Hebroni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Samsoni akalala tu hadi usiku wa manane. Akaamka, na kushika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing’oa pamoja na makomeo yake. Akaviweka mabegani mwake na kuvipeleka hadi kilele cha mlima unaokabili Hebroni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing'oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Samsoni akabaki mjini mpaka usiku wa manane. Wakati wa usiku wa manane akaamka akashika miimo miwili ya malango, akaing'oa pamoja na makomeo yake akaibeba na kwenda nayo mpaka karibu na Hebroni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Samsoni akalala mpaka usiku wa manane. Akaondoka katikati ya usiku, akashika milango ya lango la mji pamoja na miimo yake miwili, akaing'oa, makomeo yake na vyote. Akaviweka mabegani mwake na kuvipeleka mpaka kwenye kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Samsoni akalala mpaka usiku wa manane. Akaondoka katikati ya usiku, akashika milango ya lango la mji pamoja na miimo yake miwili, akaing’oa, makomeo yake na vyote. Akaviweka mabegani mwake na kuvipeleka mpaka kwenye kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Samsoni akalala hadi usiku wa manane, akaamka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing'oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hadi katika kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Samsoni akabaki mjini mpaka usiku wa manane. Wakati wa usiku wa manane akaamka akashika miimo miwili ya malango, akaingoa pamoja na makomeo yake akaibeba na kwenda nayo mpaka karibu na Hebroni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Samusoni akalala mpaka usiku wa manane tu; hapo usiku wa manane ndipo, alipoondoka, akaishika milango ya lango la mji pamoja na miimo yake miwili, akaing'oa pamoja na komeo, akajitwika mabegani, akaipandisha mlimani kunakoelekea Heburoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing’oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Samusoni akabaki katika muji mpaka saa za usiku kati. Wakati wa usiku kati akaamuka akashika miimo miwili ya mulango, akaiongoa pamoja na vifungio vyake akaibeba na kwenda nayo mpaka karibu na Hebroni.