Judges 17:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mika akamrudishia mama yake hivyo vipande 1,100 vya fedha. Mama yake akasema, “Ili laana niliyotoa isikupate, fedha hii naiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, ili kutengenezea sanamu ya kuchonga na ya kusubu. Sasa ninakurudishia vipande hivyo vya fedha.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipozirudisha zile shekeli elfu moja na mia moja za fedha kwa mama yake, mama yake akamwambia, “Mimi nimeiweka fedha hii wakfu kwa Mwenyezi Mungu ili mwanangu atengeneze sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu. Mimi nitakurudishia wewe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akamrudishia mama yake hizo fedha elfu na mia moja. Mama yake akasema, Mimi naziweka fedha hizi kabisa ziwe wakfu kwa Bwana, zitoke mkononi mwangu kwa ajili ya mwanangu, ili kufanya sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu; basi kwa hiyo nakurudishia wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mika akamrudishia mama yake hivyo vipande 1,100 vya fedha. Mama yake akasema, “Ili laana niliyotoa isikupate, fedha hii naiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, ili kutengenezea sanamu ya kuchonga na ya kusubu. Sasa ninakurudishia vipande hivyo vya fedha.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipozirudisha zile shekeli 1,100 za fedha kwa mama yake, mama yake akamwambia, “Mimi nimeiweka fedha hii wakfu kwa BWANA kwa ajili ya mwanangu kutengenezea kinyago cha kuchonga na sanamu ya kusubu. Mimi nitakurudishia wewe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipozirudisha zile shekeli 1,100 za fedha kwa mama yake, mama yake akamwambia, “Mimi nimeiweka fedha hii wakfu kwa bwana kwa ajili ya mwanangu kutengenezea kinyago cha kuchonga na sanamu ya kusubu. Mimi nitakurudishia wewe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akamrudishia mama yake hizo fedha elfu na mia moja. Mama yake akasema, Mimi naziweka fedha hizi kabisa ziwe wakfu kwa BWANA, zitoke mkononi mwangu kwa ajili ya mwanangu, ili kufanya sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu; basi kwa hiyo nakurudishia wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mika akamrudishia mama yake hivyo vipande 1,100 vya fedha. Mama yake akasema, “Ili laana niliyotoa isikupate, fedha hii naiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, ili kutengenezea sanamu ya kuchonga na ya kusubu. Sasa ninakurudishia vipande hivyo vya fedha.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamrudishia mama yake hizo fedha 1100 naye mama yake akasema: Hizi fedha nimezitoa kabisa kuwa mali za Bwana, zitoke mkononi mwangu kwa ajili ya mwanangu, atengeneze kinyago cha kuchongwa, nacho kivikwe mabati ya fedha. Kwa hiyo sasa nazirudisha kwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akamrudishia mama yake hizo fedha elfu na mia moja. Mama yake akasema, Mimi naziweka fedha hizi kabisa ziwe wakfu kwa BWANA, zitoke mkononi mwangu kwa ajili ya mwanangu, ili kufanya sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu; basi kwa hiyo nakurudishia wewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mika akamurudishia mama yake hivyo vikoroti vya feza elfu moja na mia moja. Mama yake akasema: “Kusudi laana niliyotoa isikupate, feza hii ninaitoa kwa Yawe kwa kutengeneza sanamu ya kuchonga na ya kuyeyushwa. Sasa ninakurudishia vikoroti vya feza.”