Judges 17:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kijana huyo akaondoka Bethlehemu nchini Yuda, akaenda kutafuta mahali pengine pa kuishi. Katika safari yake akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya milima ya Efraimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyu kijana akatoka mji huo wa Bethlehemu ya Yuda na kutafuta mahali pengine pa kuishi. Alipokuwa akisafiri, akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya vilima ya Efraimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu huyo akatoka katika huo mji, katika Bethlehemu-yuda, ili aende kukaa hali ya ugeni hapo atakapoona mahali; akafikilia nchi ya vilima vilima ya Efraimu katika safari yake, hata nyumba ya huyo Mika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kijana huyo akaondoka Bethlehemu nchini Yuda, akaenda kutafuta mahali pengine pa kuishi. Katika safari yake akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya milima ya Efraimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyu kijana akatoka katika mji huo wa Bethlehemu ya Yuda na kutafuta mahali pengine ambapo angeweza kuishi. Alipokuwa akisafiri, akafika nyumbani kwa Mika katika vilima vya Efraimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyu kijana akatoka katika mji huo wa Bethlehemu ya Yuda na kutafuta mahali pengine ambapo angeweza kuishi. Alipokuwa akisafiri, akafika nyumbani kwa Mika katika vilima vya Efraimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu huyo akatoka katika huo mji, Bethlehemu-yuda, ili aende kukaa kama mgeni hapo atakapoona mahali; akafikia nchi ya vilima vilima ya Efraimu katika safari yake, hadi nyumba ya huyo Mika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kijana huyo akaondoka Bethlehemu nchini Yuda, akaenda kutafuta mahali pengine pa kuishi. Katika safari yake akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya milima ya Efraimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha huyu mtu akaondoka katika mji wa Beti-Lehemu wa Yuda kwenda kukaa ugenini mahali, atakapopaona; naye akafika milimani kwa Efuraimu nyumbani kwa Mika alipokuwa anajiendea tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu huyo akatoka katika huo mji, katika Bethlehemu-yuda, ili aende kukaa hali ya ugeni hapo atakapoona mahali; akafikilia nchi ya vilima vilima ya Efraimu katika safari yake, hata nyumba ya huyo Mika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kijana huyo akaondoka Betelehemu katika inchi ya Yuda, akaenda kutafuta pahali pengine pa kuishi. Katika safari yake akafika katika nyumba ya Mika katika inchi ya milima ya Efuraimu.