Judges 18:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hizo hakukuwa na mfalme katika Israeli. Basi kabila la Dani lilikuwa linatafuta eneo lake lenyewe la kuishi humo, kwani mpaka wakati huo, halikuwa limegawiwa sehemu yake lenyewe miongoni mwa makabila ya Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku hizo, Waisraeli hawakuwa na mfalme. Katika siku hizo, watu wa kabila la Dani walikuwa wanatafuta mahali pao wenyewe pa kuishi, kwa sababu walikuwa hawajafika kwenye urithi wao miongoni mwa makabila ya Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; tena katika siku hizo kabila ya Wadani wakajitafutia urithi wapate mahali pa kukaa; maana hata siku hiyo urithi wao haujawaangukia kati ya kabila za Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hizo hakukuwa na mfalme katika Israeli. Basi kabila la Dani lilikuwa linatafuta eneo lake lenyewe la kuishi humo, kwani mpaka wakati huo, halikuwa limegawiwa sehemu yake lenyewe miongoni mwa makabila ya Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku hizo Israeli walikuwa hawana mfalme. Katika siku hizo kabila la Wadani walikuwa wanatafuta mahali pao wenyewe pa kuishi, kwa sababu walikuwa hawajafika kwenye urithi wao miongoni mwa makabila ya Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku hizo Israeli walikuwa hawana mfalme. Katika siku hizo kabila la Wadani walikuwa wanatafuta mahali pao wenyewe pa kuishi, kwa sababu walikuwa hawajafika kwenye urithi wao miongoni mwa makabila ya Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; tena katika siku hizo kabila la Wadani wakajitafutia urithi wapate mahali pa kukaa; maana hawakuwa wamepata urithi wao kati ya makabila ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hizo hakukuwa na mfalme katika Israeli. Basi kabila la Dani lilikuwa linatafuta eneo lake lenyewe la kuishi humo, kwani mpaka wakati huo, halikuwa limegawiwa sehemu yake lenyewe miongoni mwa makabila ya Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile hakuwako mfalme kwao Waisiraeli, tena siku zile wao wa shina la Dani walikuwa wanajitafutia fungu la nchi la kukaa, kwani mpaka siku hiyo fungu lao la nchi halijawaangukia katikati ya mashina ya Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; tena katika siku hizo kabila ya Wadani wakajitafutia urithi wapate mahali pa kukaa; maana hata siku hiyo urithi wao haujawaangukia kati ya kabila za Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku zile hakukukuwa mufalme katika Israeli. Basi kabila la Dani lilikuwa linatafuta eneo lake lenyewe la kuishi ndani yake, maana mpaka wakati ule, halikukuwa limegawanyiwa sehemu yake lenyewe kati ya makabila ya Israeli.