Judges 18:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtakapofika huko mtakuta watu wasio na wasiwasi wowote. Nchi hiyo ni kubwa, haikupungukiwa chochote na Mungu ameitia mikononi mwetu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtakapofika huko, mtawakuta watu walio salama, na nchi kubwa ambayo Mungu ameitia mikononi mwenu, isiyopungukiwa kitu chochote duniani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapo mtakapokwenda mtawafikilia watu wakaao salama salimini, na hiyo nchi nayo ni kubwa; kwa kuwa Mungu ameitia mikononi mwenu; ni mahali ambapo hapana kupungukiwa na kitu cho chote kilicho duniani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtakapofika huko mtakuta watu wasio na wasiwasi wowote. Nchi hiyo ni kubwa, haikupungukiwa chochote na Mungu ameitia mikononi mwetu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtakapokwenda huko mtakuta watu waliotulia walio salama, nayo nchi hiyo ni kubwa na Mungu ameitia mikononi mwenu, nayo ni nchi ambayo haikupungukiwa na kitu cho chote kilicho duniani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtakapokwenda huko mtakuta watu waliotulia walio salama, nayo nchi hiyo ni kubwa na Mungu ameitia mikononi mwenu, nayo ni nchi ambayo haikupungukiwa na kitu chochote kilicho duniani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hapo mtakapokwenda mtawafikia watu wakaao kwa amani, na hiyo nchi nayo ni kubwa; kwa kuwa Mungu ameitia mikononi mwenu; ni mahali ambapo hapapungukiwi na kitu chochote kilichoko duniani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtakapofika huko mtakuta watu wasio na wasiwasi wowote. Nchi hiyo ni kubwa, haikupungukiwa chochote na Mungu ameitia mikononi mwetu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtakapofika mtafika kwenye watu wanaokaa na kutulia, nayo nchi hiyo inapanuka pande mbili. Kweli Mungu ameitia mikononi mwenu, tena ni mahali pasipokoseka lo lote lililoko huku nchini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapo mtakapokwenda mtawafikilia watu wakaao salama salimini, na hiyo nchi nayo ni kubwa; kwa kuwa Mungu ameitia mikononi mwenu; ni mahali ambapo hapana kupungukiwa na kitu cho chote kilicho duniani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutakapofika kule mutakuta watu wasiokuwa na wasiwasi wowote. Inchi hiyo ni kubwa, haikupungukiwa chochote, na Mungu ameitia katika mikono yetu.”