Judges 18:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wale watano waliokwenda kuipeleleza nchi ya Laishi wakawaambia ndugu zao, “Je, mnajua kwamba katika nyumba mojawapo ya hizi kuna kizibao, kinyago na sanamu ya kusubu? Basi, fikirini namna ya kufanya.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wale wanaume watano waliopeleleza nchi ya Laishi wakawaambia ndugu zao, “Je, mnajua kuwa katika mojawapo ya nyumba hizi kuna kizibau, miungu ya nyumbani, sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu? Sasa basi, fikirini mtakalofanya.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo hao watu watano waliokwenda kuipeleleza nchi ya Laisha wakajibu, na kuwaambia ndugu zao Je! Ninyi mwajua ya kwamba mna naivera ndani ya nyumba hizi, na kinyago na sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu? Basi sasa fikirini iwapasayo kufanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wale watano waliokwenda kuipeleleza nchi ya Laishi wakawaambia ndugu zao, “Je, mnajua kwamba katika nyumba mojawapo ya hizi kuna kizibao, kinyago na sanamu ya kusubu? Basi, fikirini namna ya kufanya.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wale watu watano waliopeleleza nchi ya Laishi wakawaambia ndugu zao, “Je, mwajua kuwa mojawapo ya nyumba hizi kuna naivera, sanamu ndogo za nyumbani, sanamu ya kuchonga na sanamu ya kusubu? Sasa basi fikirieni mtakalofanya.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wale watu watano waliopeleleza nchi ya Laishi wakawaambia ndugu zao, “Je, mwajua kuwa mojawapo ya nyumba hizi kuna naivera, sanamu ndogo za nyumbani, sanamu ya kuchonga na sanamu ya kusubu? Sasa basi fikirini mtakalofanya.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo hao watu watano waliokwenda kuipeleleza nchi ya Laisha wakawaambia ndugu zao, Je! Ninyi mwajua ya kwamba mna naivera ndani ya nyumba hizi, na kinyago na sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu? Basi sasa fikirini iwapasavyo kufanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wale watano waliokwenda kuipeleleza nchi ya Laishi wakawaambia ndugu zao, “Je, mnajua kwamba katika nyumba mojawapo ya hizi kuna kizibao, kinyago na sanamu ya kusubu? Basi, fikirini namna ya kufanya.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wale watu watano waliokwenda kuipeleleza nchi ya Laisi wakaanza kusema na ndugu zao, wakawaambia: Je? Mnajua, ya kuwa humu katika hizi nyumba kimo kisibau cha mtambikaji pamoja na kinyago cha nyumbani, nacho ni inyago cha kuchongwa kilichovikwa mabati ya fedha. Sasa lijueni la kufanya!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo hao watu watano waliokwenda kuipeleleza nchi ya Laisha wakajibu, na kuwaambia ndugu zao Je! Ninyi mwajua ya kwamba mna naivera ndani ya nyumba hizi, na kinyago na sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu? Basi sasa fikirini iwapasayo kufanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wale watano waliokwenda kuipeleleza inchi ya Laisi wakawaambia wandugu zao: “Munajua kwamba katika nyumba moja kati ya hizi kuna kizibao, sanamu ya kuchongwa na sanamu yenye kuyeyushwa? Basi, mufikiri namna ya kufanya.”