Judges 18:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale watu watano waliokwenda kuipeleleza nchi waliingia ndani, wakachukua ile sanamu mungu ya kusubu, kile kizibao na kinyago cha ibada. Wakati huo yule kuhani alikuwa amesimama mlangoni pamoja na wale watu 600 wenye silaha. Basi, alipowaona wale wapelelezi
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale watu watano walioenda kupeleleza nchi wakaingia ndani na kuchukua ile sanamu ya kuchonga, kile kizibau, na ile miungu ya nyumbani, na ile sanamu ya kusubu, wakati yule kuhani akiwa amesimama pale penye ingilio la lango pamoja na wale watu mia sita waliojifunga silaha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao watu watano waliokwenda kuipeleleza hiyo nchi wakakwea juu, wakaingia ndani, na kuitwaa hiyo sanamu ya kuchonga, na hiyo naivera, na kile kinyago, na hiyo sanamu ya kusubu; na huyo kuhani akasimama penye maingilio ya lango pamoja na hao watu waume sita mia wenye kuvaa silaha za vita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale watu watano waliokwenda kuipeleleza nchi waliingia ndani, wakachukua ile sanamu mungu ya kusubu, kile kizibao na kinyago cha ibada. Wakati huo yule kuhani alikuwa amesimama mlangoni pamoja na wale watu 600 wenye silaha. Basi, alipowaona wale wapelelezi
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale watu watano waliokwenda kupeleleza nchi wakaingia ndani na kuchukua ile sanamu ya kuchonga, ile naivera, ndiyo kisibau cha kuhani, zile sanamu nyingine ndogo za nyumbani pamoja na ile sanamu ya kusubu, wakati yule kuhani akiwa amesimama pale penye ingilio la lango pamoja na wale watu 600 waliokuwa wamejifunga silaha za vita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale watu watano waliokwenda kupeleleza nchi wakaingia ndani na kuchukua ile sanamu ya kuchonga, ile naivera, na zile sanamu nyingine ndogo za nyumbani pamoja na ile sanamu ya kusubu, wakati yule kuhani akiwa amesimama pale penye ingilio la lango pamoja na wale watu 600 waliokuwa wamejifunga silaha za vita.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao watu watano waliokwenda kuipeleleza hiyo nchi wakakwea juu, wakaingia ndani, na kuitwaa hiyo sanamu ya kuchonga, na hiyo naivera, na kile kinyago, na hiyo sanamu ya kusubu; na huyo kuhani akasimama penye maingilio ya lango pamoja na hao wanaume mia sita wenye kuvaa silaha za vita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale watu watano waliokwenda kuipeleleza nchi waliingia ndani, wakachukua ile sanamu mungu ya kusubu, kile kizibao na kinyago cha ibada. Wakati huo yule kuhani alikuwa amesimama mlangoni pamoja na wale watu 600 wenye silaha. Basi, alipowaona wale wapelelezi
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wale watu watano waliokwenda kuipeleleza nchi hii wakaingia humo, wakakichukua kile kinyago cha kuchongwa pamoja na kisibau cha mtambikaji, ni kile kinyago cha nyumbani kilichovikwa mabati ya fedha, naye mtambikaji alikuwa amesimama pa kuingia langoni kwao wale watu 600 waliojifunga mata ya kupigia vita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao watu watano waliokwenda kuipeleleza hiyo nchi wakakwea juu, wakaingia ndani, na kuitwaa hiyo sanamu ya kuchonga, na hiyo naivera, na kile kinyago, na hiyo sanamu ya kusubu; na huyo kuhani akasimama penye maingilio ya lango pamoja na hao watu waume sita mia wenye kuvaa silaha za vita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale watu watano waliokwenda kuipeleleza inchi wakaingia ndani, wakabeba ile sanamu ya mungu yenye kuyeyushwa, kile kizibao na sanamu ya ibada. Wakati ule yule kuhani alikuwa akisimama kwenye mulango pamoja na wale watu mia sita wenye silaha.