Judges 18:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao wakamwambia, “Nyamaza, funga mdomo wako, uje pamoja nasi, uwe kuhani wetu na kama baba yetu. Au waonaje? Je, yafaa kwako zaidi kuwa kuhani wa mtu mmoja ama kuwa kuhani wa kabila moja la Israeli?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamjibu, “Nyamaza! Weka mkono wako juu ya kinywa chako na ufuatane nasi, uwe baba yetu na kuhani wetu. Si ni afadhali utumikie kabila na ukoo katika Israeli kama kuhani kuliko kumtumikia mtu mmoja na watu wa nyumbani mwake?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wao wakamwambia, Nyamaza wewe, weka mkono wako kinywani mwako, uende pamoja nasi, uwe kwetu baba, tena kuhani; je! Ni vema kwako kuwa kuhani kwa ajili ya nyumba ya mtu mmoja, au kuwa kuhani kwa ajili ya kabila na jamaa katika Israeli?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao wakamwambia, “Nyamaza, funga mdomo wako, uje pamoja nasi, uwe kuhani wetu na kama baba yetu. Au waonaje? Je, yafaa kwako zaidi kuwa kuhani wa mtu mmoja ama kuwa kuhani wa kabila moja la Israeli?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamjibu, “Nyamaza kimya! Weka mkono wako juu ya kinywa chako na ufuatane nasi, uwe baba yetu na kuhani wetu. Si ni afadhali utumikie kabila na ukoo katika Israeli kama kuhani kuliko kumtumikia mtu mmoja na watu wa nyumbani mwake?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamjibu, “Nyamaza kimya! Weka mkono wako juu ya kinywa chako na ufuatane nasi, uwe baba yetu na kuhani wetu. Si ni afadhali utumikie kabila na ukoo katika Israeli kama kuhani kuliko kumtumikia mtu mmoja na watu wa nyumbani mwake?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wao wakamwambia, Nyamaza wewe, weka mkono wako kinywani mwako, uende pamoja nasi, uwe kwetu baba, tena kuhani; je! Ni vema kwako kuwa kuhani kwa ajili ya nyumba ya mtu mmoja, au kuwa kuhani kwa ajili ya kabila na jamaa katika Israeli?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao wakamwambia, “Nyamaza, funga mdomo wako, uje pamoja nasi, uwe kuhani wetu na kama baba yetu. Au waonaje? Je, yafaa kwako zaidi kuwa kuhani wa mtu mmoja ama kuwa kuhani wa kabila moja la Israeli?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wao wakamwambia: Nyamaza tu ukiubandika mkono wako kinywani pako, upate kwenda nasi kuwa baba yetu na mtambikaji wetu. Ni vema, ukiwa mtambikaji wa mlango wa mtu mmoja, kuliko ukiwa mtambikaji wa shina na wa ukoo mzima kwao Waisiraeli?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wao wakamwambia, Nyamaza wewe, weka mkono wako kinywani mwako, uende pamoja nasi, uwe kwetu baba, tena kuhani; je! Ni vema kwako kuwa kuhani kwa ajili ya nyumba ya mtu mmoja, au kuwa kuhani kwa ajili ya kabila na jamaa katika Israeli?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakamwambia: “Nyamaza, funga kinywa chako, ukuje pamoja nasi, ukuwe kuhani wetu na kama baba yetu. Au unaona namna gani? Inafaa kwako zaidi kuwa kuhani wa mutu mumoja au kuwa kuhani wa kabila moja la Israeli?”