Judges 18:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo watu wa kabila la Dani walichagua miongoni mwao watu hodari wakawatuma kutoka huko Eshtaoli na Sora wakawaamuru waende kuipeleleza nchi. Basi watu hao wakafika katika nchi ya milima ya Efraimu, nyumbani kwa Mika, wakakaa humo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Wadani wakatuma mashujaa watano kutoka Sora na Eshtaoli ili kupeleleza nchi na kuichunguza. Hawa mashujaa waliwakilisha koo zao zote. Waliwaambia, “Nendeni mkaichunguze hiyo nchi.” Wanaume hao wakaingia katika nchi ya vilima ya Efraimu, wakafika nyumba ya Mika, ambako walilala usiku huo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wana wa Dani wakatuma watu wa jamaa zao, watu watano katika hesabu yao yote, watu mashujaa, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli, ili kuipeleleza hiyo nchi, kuiaua; wakawaambia, Haya, endeni mkaikague nchi hii; basi wakaifikilia nchi ya vilima vilima ya Efraimu, hata nyumba ya huyo Mika, Wakalala huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo watu wa kabila la Dani walichagua miongoni mwao watu hodari wakawatuma kutoka huko Eshtaoli na Sora wakawaamuru waende kuipeleleza nchi. Basi watu hao wakafika katika nchi ya milima ya Efraimu, nyumbani kwa Mika, wakakaa humo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Wadani wakatuma mashujaa watano kutoka Sora na Eshtaoli ili kupeleleza nchi na kuichunguza. Hawa watu waliwakilisha koo zao zote. Wao waliwaambia, “Nendeni mkaichuguze hiyo nchi.” Hao watu wakaingia katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao wakafika kwenye nyumba ya Mika, ambako walilala usiku huo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Wadani wakatuma mashujaa watano kutoka Sora na Eshtaoli ili kupeleleza nchi na kuichunguza. Hawa watu waliwakilisha koo zao zote. Waliwaambia, “Nendeni mkaichunguze hiyo nchi.” Watu hao wakaingia katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao wakafika nyumba ya Mika, ambako walilala usiku huo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wana wa Dani wakatuma watu watano kutoka kwa koo zao zote, watu mashujaa, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli, ili kuipeleleza hiyo nchi, kuikagua; wakawaambia, Haya, endeni mkaikague nchi hii; basi wakaifikia nchi ya vilima vilima ya Efraimu, hadi nyumba ya huyo Mika, Wakalala huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo watu wa kabila la Dani walichagua miongoni mwao watu hodari wakawatuma kutoka huko Eshtaoli na Sora wakawaamuru waende kuipeleleza nchi. Basi watu hao wakafika katika nchi ya milima ya Efraimu, nyumbani kwa Mika, wakakaa humo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo wana wa Dani wakatoa katika ukoo wao wote mzima watu watano wenye nguvu waliokuwa wa Sora na wa Estaoli, wakawatuma kuipeleleza nchi na kuichunguza wakiwaambia: Nendeni mwichunguze nchi hii! Walipofika milimani kwa Efuraimu kwenye nyumba ya Mika wakalala huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wana wa Dani wakatuma watu wa jamaa zao, watu watano katika hesabu yao yote, watu mashujaa, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli, ili kuipeleleza hiyo nchi, kuiaua; wakawaambia, Haya, endeni mkaikague nchi hii; basi wakaifikilia nchi ya vilima vilima ya Efraimu, hata nyumba ya huyo Mika, Wakalala huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo watu wa kabila la Dani wakachagua kati yao watu hodari, wakawatuma kutoka kule Estaoli na Zora, wakawaamuru waende kuipeleleza inchi. Basi watu hao wakafika katika inchi ya milima ya Efuraimu katika nyumba ya Mika, wakaenda na kukaa mule.