Judges 18:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakaanza safari yao, huku wametanguliwa na watoto wao na mifugo na mali zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wakageuka na kuondoka, wakiwatanguliza mbele watoto wao wadogo, mifugo na mali yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakageuka wakaenda zao, lakini watoto wadogo na wanyama wao wa mifugo, na vyombo vyao, wakawatanguliza mbele yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakaanza safari yao, huku wametanguliwa na watoto wao na mifugo na mali zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wakageuka na kuondoka wakiwatanguliza mbele watoto wao wadogo, wanyama wao wa kufugwa na mali zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wakageuka na kuondoka wakiwatanguliza mbele watoto wao wadogo, wanyama wao wa kufugwa na mali zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakageuka wakaenda zao, lakini watoto wadogo na wanyama wao wa kufugwa, na vyombo vyao, wakawatanguliza mbele yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakaanza safari yao, huku wametanguliwa na watoto wao na mifugo na mali zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakageuka kwenda zao; lakini wanawake pamoja na watoto na nyama wa kufuga na vyombo vilivyokuwa mali walitangulia mbele yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakageuka wakaenda zao, lakini watoto wadogo na wanyama wao wa mifugo, na vyombo vyao, wakawatanguliza mbele yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wakaanza safari yao, na walikuwa wanatanguliwa na watoto wao na nyama wao na mali zao.