Judges 18:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao watu wa kabila la Dani walivichukua vitu vile ambavyo Mika alikuwa amevitengeneza, wakamchukua na yule kuhani aliyemhudumia. Basi wakaenda kushambulia Laishi wakawaua wakazi wake ambao waliishi humo kwa utulivu na bila wasiwasi, wakauteketeza mji huo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wakachukua vitu vile Mika alikuwa amevitengeneza, na kuhani wake, wakaendelea hadi Laishi, dhidi ya watu walioishi na amani na utulivu. Wakawashambulia kwa upanga na kuuteketeza mji wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakakitwaa hicho alichokuwa amekifanya Mika, na kuhani aliyekuwa naye nao wakafikilia Laisha, kwenye watu waliokuwa wenye starehe na hifadhi, wakawapiga kwa makali ya upanga; wakaupiga moto mji wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao watu wa kabila la Dani walivichukua vitu vile ambavyo Mika alikuwa amevitengeneza, wakamchukua na yule kuhani aliyemhudumia. Basi wakaenda kushambulia Laishi wakawaua wakazi wake ambao waliishi humo kwa utulivu na bila wasiwasi, wakauteketeza mji huo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wakachukua vile Mika alivyokuwa ametengeneza pamoja na kuhani wake, wakaendelea hadi Laishi, dhidi ya watu walio na amani wasiokuwa na wasiwasi. Wakawashambulia kwa upanga na kuuteketeza mji wao kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wakachukua vile Mika alivyokuwa ametengeneza, na kuhani wake, wakaendelea hadi Laishi, dhidi ya watu walio na amani, wasiokuwa na wasiwasi. Wakawashambulia kwa upanga na kuuteketeza mji wao kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakakitwaa hicho alichokuwa amekifanya Mika, na kuhani aliyekuwa naye nao wakafika Laisha, kwa watu waliokuwa watulivu na wasioshuku, wakawapiga kwa makali ya upanga; wakauteketeza kwa moto mji wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao watu wa kabila la Dani walivichukua vitu vile ambavyo Mika alikuwa amevitengeneza, wakamchukua na yule kuhani aliyemhudumia. Basi wakaenda kushambulia Laishi wakawaua wakazi wake ambao waliishi humo kwa utulivu na bila wasiwasi, wakauteketeza mji huo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakavichukua vile, Mika alivyovitengeneza, pamoja na mtambikaji aliyekuwa kwake, wakaenda Laisi, kwenye wale watu waliokaa kimya na kutulia tu, wakawapiga kwa ukali wa panga, nao mji wakauteketeza kwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakakitwaa hicho alichokuwa amekifanya Mika, na kuhani aliyekuwa naye nao wakafikilia Laisha, kwenye watu waliokuwa wenye starehe na hifadhi, wakawapiga kwa makali ya upanga; wakaupiga moto mji wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao watu wa kabila la Dani walivitwaa vitu vile ambavyo Mika alikuwa amevitengeneza, na kumupeleka yule kuhani aliyemutumikia. Basi wakaenda kushambulia muji wa Laisi, wakawaua wakaaji wake ambao waliishi mule kwa utulivu na bila wasiwasi, wakauteketeza muji ule.