Judges 18:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakazi wa mji huo hawakuwa na mtu wa kuwaokoa kwa sababu walikuwa mbali na mji wa Sidoni, tena hawakuwa na uhusiano na watu wengine. Mji huo ulikuwa kwenye bonde la Beth-rehobu. Watu wa kabila la Dani wakaujenga upya, wakaishi humo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hapakuwa na yeyote wa kuwaokoa, kwa kuwa waliishi mbali na Sidoni, na hawakuwa na ushirikiano na mtu mwingine yeyote. Mji huo ulikuwa kwenye bonde karibu na Beth-Rehobu. Wadani wakaujenga upya huo mji na kuishi humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hakuwako mwokozi, kwa sababu huo mji ulikuwa ni mbali sana na Sidoni, nao hawakuwa na shughuli na mtu awaye yote; na mji huo ulikuwa katika hilo bonde lililo karibu na Bethrehobu. Nao wakaujenga huo mji na kukaa humo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakazi wa mji huo hawakuwa na mtu wa kuwaokoa kwa sababu walikuwa mbali na mji wa Sidoni, tena hawakuwa na uhusiano na watu wengine. Mji huo ulikuwa kwenye bonde la Beth-rehobu. Watu wa kabila la Dani wakaujenga upya, wakaishi humo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hapakuwepo na ye yote wa kuwaokoa, kwa kuwa kulikuwa mbali sana na Sidoni na hawakuwa na ushirikiano na mtu mwingine ye yote. Mji ulikuwa kwenye bonde karibu na Beth-Rehobu. Wadani wakaujenga upya huo mji na kuishi humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hapakuwa na yeyote wa kuwaokoa, kwa kuwa kulikuwa mbali sana na Sidoni na hawakuwa na ushirikiano na mtu mwingine yeyote. Mji ulikuwa kwenye bonde karibu na Beth-Rehobu. Wadani wakaujenga upya huo mji na kuishi humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hakukuwa na mwokozi, kwa sababu huo mji ulikuwa mbali sana na Sidoni, nao hawakutangamana na watu wowote wale; na mji huo ulikuwa katika hilo bonde lililo karibu na Bethrehobu. Nao wakaujenga huo mji na kukaa humo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakazi wa mji huo hawakuwa na mtu wa kuwaokoa kwa sababu walikuwa mbali na mji wa Sidoni, tena hawakuwa na uhusiano na watu wengine. Mji huo ulikuwa kwenye bonde la Beth-rehobu. Watu wa kabila la Dani wakaujenga upya, wakaishi humo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hakuwako aliyewaponya, kwani kwenda Sidoni toka kwao kulikuwa mbali, nao walikuwa hawana matata na watu wo wote; nao mji wao ulikuwa bondeni kuelekea Beti-Rehobu. Kisha wakaujenga huo mji tena, wakakaa humo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hakuwako mwokozi, kwa sababu huo mji ulikuwa ni mbali sana na Sidoni, nao hawakuwa na shughuli na mtu awaye yote; na mji huo ulikuwa katika hilo bonde lililo karibu na Bethrehobu. Nao wakaujenga huo mji na kukaa humo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaaji wa muji ule hawakukuwa na mutu wa kuwaokoa kwa sababu walikuwa mbali na muji wa Sidona, tena hawakukuwa na ushirika na watu wengine. Muji ule ulikuwa kwenye bonde la Beti-Rehobu. Watu wa kabila la Dani wakaujenga upya, wakaishi mule.