Judges 18:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, watu hao watano wakaondoka, wakaenda Laishi. Waliwaona watu walioishi huko, na jinsi walivyokaa kwa usalama kama vile watu wa Sidoni. Walikuwa watu watulivu wasio na wasiwasi na hawakupungukiwa mahitaji yoyote nchini. Walikuwa mbali na watu wa Sidoni, na hawakuwa na shughuli yoyote na watu wengine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi hao wanaume watano wakaondoka na kufika Laishi, mahali ambapo waliwakuta watu wanaishi salama, kama Wasidoni, kwa amani na utulivu. Nchi yao haikupungukiwa kitu, hivyo wakastawi. Pia walikaa mbali sana na Wasidoni, wala hawakushughulika na mtu yeyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo hao watu watano wakaenda zao, wakafika Laisha, wakawaona wale watu waliokuwamo ndani yake, jinsi walivyokaa salama salimini kwa mfano wa walivyokaa hao Wasidoni, wenye starehe na hifadhi, kwa maana hapakuwa na mtu katika nchi hiyo aliyekuwa na amri, aliyeweza kuwatweza katika neno lo lote, nao walikuwa wa mbali na hao Wasidoni, wala hawakuwa na shughuli na mtu ye yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, watu hao watano wakaondoka, wakaenda Laishi. Waliwaona watu walioishi huko, na jinsi walivyokaa kwa usalama kama vile watu wa Sidoni. Walikuwa watu watulivu wasio na wasiwasi na hawakupungukiwa mahitaji yoyote nchini. Walikuwa mbali na watu wa Sidoni, na hawakuwa na shughuli yoyote na watu wengine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi hao watu watano wakaondoka na kufika Laishi, mahali ambapo waliwakuta watu wanaishi kwa amani na salama, kama Wasidoni, kwa utulivu na bila mashaka, bila kupungukiwa na kitu cho chote duniani, wakiwa na utajiri. Nao walikaa mbali na Wasidoni wala hawakushughulika na mtu ye yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi hao watu watano wakaondoka na kufika Laishi, mahali ambapo waliwakuta watu wanaishi salama, kama Wasidoni, kwa utulivu na bila mashaka. Nchi yao haikupungukiwa na kitu chochote, hivyo wakawa tajiri. Pia walikaa mbali sana na Wasidoni, wala hawakushughulika na mtu yeyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo hao watu watano wakaenda zao, wakafika Laisha, wakawaona wale watu waliokuwamo ndani yake, jinsi walivyokaa kwa amani, kama ilivyokuwa desturi ya Wasidoni, watu watulivu na wasioshuku, wasiopungukiwa na chochote duniani, na waliokuwa na miliki; Nao walikuwa mbali na hao Wasidoni, wala hawakutangamana na watu wengine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, watu hao watano wakaondoka, wakaenda Laishi. Waliwaona watu walioishi huko, na jinsi walivyokaa kwa usalama kama vile watu wa Sidoni. Walikuwa watu watulivu wasio na wasiwasi na hawakupungukiwa mahitaji yoyote nchini. Walikuwa mbali na watu wa Sidoni, na hawakuwa na shughuli yoyote na watu wengine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hao watu watano walipokwenda zao wakafika Laisi, wakaona, ya kuwa watu waliokuwamo walikaa na kutulia tu kama desturi za Wasidoni, walikaa kimya na kutulia kweli, kwani hakuwako katika nchi hiyo aliyewafanyizia kibaya cho chote, nao wote walikuwa wenye mali. Tena kutoka kwa Wasidoni kufika kwao kulikuwa mbali, hawakupata matata yo yote na watu wo wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo hao watu watano wakaenda zao, wakafika Laisha, wakawaona wale watu waliokuwamo ndani yake, jinsi walivyokaa salama salimini kwa mfano wa walivyokaa hao Wasidoni, wenye starehe na hifadhi, kwa maana hapakuwa na mtu katika nchi hiyo aliyekuwa na amri, aliyeweza kuwatweza katika neno lo lote, nao walikuwa wa mbali na hao Wasidoni, wala hawakuwa na shughuli na mtu ye yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, watu hao watano wakaondoka, wakaenda Laisi. Waliwaona watu walioishi kule, na jinsi walivyokaa kwa usalama kama vile watu wa Sidona. Walikuwa watu watulivu wasiokuwa na wasiwasi na hawakupungukiwa mahitaji yoyote katika inchi. Walikuwa mbali na watu wa Sidona, na hawakukuwa na shuguli yoyote na watu wengine.