Judges 19:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini huyo mtu alikataa kulala huko usiku huo. Basi, akainuka, akaondoka akafika karibu na mji wa Yebusi (yaani Yerusalemu). Alikuwa na wale punda wake wawili waliotandikwa tayari, pamoja na suria wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini akakataa kulala tena, akaondoka na kuelekea Yebusi (ndio Yerusalemu), akiwa na punda wake wawili waliotandikwa, pamoja na suria wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini huyo mtu hakukubali kukaa usiku huo, ila akainuka, akaenda zake, akafika mkabala wa Yebusi (huo ndio Yerusalemu); nao walikuwako pamoja naye punda wawili waliotandikwa; suria yake naye alikuwa pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini huyo mtu alikataa kulala huko usiku huo. Basi, akainuka, akaondoka akafika karibu na mji wa Yebusi (yaani Yerusalemu). Alikuwa na wale punda wake wawili waliotandikwa tayari, pamoja na suria wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini akakataa kulala tena, akaondoka na kwenda mpaka Yebusi (ndio Yerusalemu), akiwa na punda wake wawili waliotandikiwa, pamoja na suria wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini akakataa kulala tena, akaondoka na kwenda mpaka Yebusi (ndio Yerusalemu), akiwa na punda wake wawili waliotandikiwa, pamoja na suria wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini huyo mtu hakukubali kukaa usiku huo, ila akainuka, akaenda zake, akafika mkabala wa Yebusi (huo ndio Yerusalemu); nao walikuwako pamoja naye punda kadhaa waliotandikwa; suria wake naye alikuwa pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini huyo mtu alikataa kulala huko usiku huo. Basi, akainuka, akaondoka akafika karibu na mji wa Yebusi (yaani Yerusalemu). Alikuwa na wale punda wake wawili waliotandikwa tayari, pamoja na suria wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yule mtu hakutaka kulala tena, akaondoka, akaenda zake, akafika ng'ambo ya Yebusi, ndio Yerusalemu; naye alikuwa na punda wake wawili waliotandikwa, hata suria yake alikuwa naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini huyo mtu hakukubali kukaa usiku huo, ila akainuka, akaenda zake, akafika mkabala wa Yebusi (huo ndio Yerusalemu); nao walikuwako pamoja naye punda wawili waliotandikwa; suria yake naye alikuwa pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini yule mutu akakataa kulala kule usiku ule. Basi, akasimama, akaondoka, akafika karibu na muji wa Yebusi, ni kusema Yerusalema. Alikuwa na wale punda wake wawili waliotandikwa tayari, pamoja na habara yake.