Judges 19:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokuwa huko mzee mmoja akafika kutoka shambani kwake. Mzee huyo alikuwa mwenyeji wa nchi ya milima ya Efraimu na alikuwa akiishi huko Gibea kama mgeni. Wakazi wa mji wa Gibea walikuwa wa kabila la Benyamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jioni ile, mzee mmoja toka nchi ya vilima ya Efraimu, aliyekuwa anaishi huko Gibea (watu wa sehemu ile walikuwa Wabenyamini), akarudi kutoka kwenye kazi zake za shamba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha, tazama, akatokea mtu mume mzee, atoka kazini kwake shambani, wakati wa jioni; mtu huyo alikuwa ni wa ile nchi ya vilima vilima ya Efraimu, naye alikuwa anakaa katika Gibea hali ya ugeni lakini wenyeji wa mahali hapo walikuwa Wabenyamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokuwa huko mzee mmoja akafika kutoka shambani kwake. Mzee huyo alikuwa mwenyeji wa nchi ya milima ya Efraimu na alikuwa akiishi huko Gibea kama mgeni. Wakazi wa mji wa Gibea walikuwa wa kabila la Benyamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jioni ile mtu mmoja mzee toka nchi ya vilima ya Efraimu, aliyekuwa anaishi huko Gibea (watu wa sehemu ile walikuwa Wabenyamini), akarudi kutoka kwenye kazi za shamba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jioni ile mtu mmoja mzee toka nchi ya vilima ya Efraimu, aliyekuwa anaishi huko Gibea (watu wa sehemu ile walikuwa Wabenyamini), akarudi kutoka kwenye kazi za shamba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha, tazama, akatokea mtu mume mzee, akitoka kazini kwake shambani, wakati wa jioni; mtu huyo alikuwa ni wa ile nchi ya vilima vilima ya Efraimu, naye alikuwa anakaa katika Gibea kama mgeni lakini wenyeji wa mahali hapo walikuwa Wabenyamini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokuwa huko mzee mmoja akafika kutoka shambani kwake. Mzee huyo alikuwa mwenyeji wa nchi ya milima ya Efraimu na alikuwa akiishi huko Gibea kama mgeni. Wakazi wa mji wa Gibea walikuwa wa kabila la Benyamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara wakaona mzee aliyechelewa, naye akatoka kazini kwake shambani; naye mtu huyu alikuwa wa milimani kwa Efuraimu, humo Gibea alikaa ugenini, maana wenyeji wa hapa walikuwa wana wa Benyamini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha, tazama, akatokea mtu mume mzee, atoka kazini kwake shambani, wakati wa jioni; mtu huyo alikuwa ni wa ile nchi ya vilima vilima ya Efraimu, naye alikuwa anakaa katika Gibea hali ya ugeni lakini wenyeji wa mahali hapo walikuwa Wabenyamini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokuwa kule muzee mumoja akafika kutoka kwa shamba lake. Muzee huyo alikuwa mutu wa inchi ya milima ya Efuraimu na alikuwa akiishi kule Gibea kama mugeni. Wakaaji wa muji wa Gibea walikuwa wa kabila la Benjamina.