Judges 19:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akamjibu, “Tumetoka Bethlehemu nchini Yuda na tunaelekea sehemu za mbali za eneo la milima ya Efraimu. Huko ndiko ninakoishi na sasa ninarudi safarini huko Bethlehemu katika Yuda na kurejea nyumbani; hakuna mtu hapa aliyetukaribisha nyumbani kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwambia, “Tumepita kutoka Bethlehemu ya Yuda, tunaelekea katika nchi ya vilima ya Efraimu ninakoishi. Nilienda Bethlehemu ya Yuda na sasa ninaenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu. Hakuna mtu yeyote aliyenikaribisha katika nyumba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia, Sisi twapita hapa kutoka Bethlehemu-yuda, twaenda huko upande wa mbali wa nchi ya vilima vilima ya Efraimu; ndiko nilikotoka nami nilikwenda Bethlehemu-yuda; nami sasa naiendea nyumba ya Bwana wala hapana mtu anikaribishaye nyumbani mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akamjibu, “Tumetoka Bethlehemu nchini Yuda na tunaelekea sehemu za mbali za eneo la milima ya Efraimu. Huko ndiko ninakoishi na sasa ninarudi safarini huko Bethlehemu katika Yuda na kurejea nyumbani; hakuna mtu hapa aliyetukaribisha nyumbani kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwambia, “Tumepita kutoka Bethlehemu ya Yuda, tunaelekea katika nchi ya vilima ya Efraimu, ambako ndiko ninakoishi. Nilikwenda Bethlehemu ya Yuda na sasa ninakwenda katika nyumba ya BWANA. Hakuna mtu ye yote aliyenikaribisha katika nyumba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwambia, “Tumepita kutoka Bethlehemu ya Yuda, tunaelekea katika nchi ya vilima ya Efraimu, ambako ndiko ninakoishi. Nilikwenda Bethlehemu ya Yuda na sasa ninakwenda katika nyumba ya bwana. Hakuna mtu yeyote aliyenikaribisha katika nyumba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia, Sisi tunapita hapa kutoka Bethlehemu-yuda, tunaenda huko upande wa mbali wa nchi ya vilima vilima ya Efraimu; ndiko nilikotoka nami nilikwenda Bethlehemu-yuda; nami sasa naiendea nyumba ya BWANA, wala hakuna mtu anikaribishaye nyumbani mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akamjibu, “Tumetoka Bethlehemu nchini Yuda na tunaelekea sehemu za mbali za eneo la milima ya Efraimu. Huko ndiko ninakoishi na sasa ninarudi safarini huko Bethlehemu katika Yuda na kurejea nyumbani; hakuna mtu hapa aliyetukaribisha nyumbani kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwambia: Sisi tu wapitaji; tumetoka Beti-Lehemu wa Yuda, tunakwenda huko ndani milimani kwa Efuraimu, ndiko, nilikotoka; nalikwenda Beti-Lehemu wa Yuda, na sasa ninakwenda nyumbani mwa Bwana, lakini hakuna mtu aliyenikaribisha nyumbani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia, Sisi twapita hapa kutoka Bethlehemu-yuda, twaenda huko upande wa mbali wa nchi ya vilima vilima ya Efraimu; ndiko nilikotoka nami nilikwenda Bethlehemu-yuda; nami sasa naiendea nyumba ya BWANA wala hapana mtu anikaribishaye nyumbani mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akamujibu: “Tunatoka Betelehemu katika inchi ya Yuda na tunaelekea sehemu za mbali za eneo la milima ya Efuraimu. Kule ndiko ninakoishi na sasa ninarudi katika safari toka kule Betelehemu katika Yuda na kurudia kwangu; hakuna mutu hapa aliyetukaribisha katika nyumba yake.