Judges 19:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo mzee akamwambia, “Amani iwe nanyi! Nitawapa mahitaji yote. Ila msilale huku uwanjani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mzee akawaambia, “Amani iwe kwenu! Karibuni nyumbani mwangu. Nitawapa mahitaji yenu yote, ila tu msilale katika uwanja huu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha huyo mzee alisema, Na iwe amani kwako; lakini na haya yaliyokupungukia na yawe juu yangu mimi lakini usilale njiani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo mzee akamwambia, “Amani iwe nanyi! Nitawapa mahitaji yote. Ila msilale huku uwanjani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mzee akawaambia, “Amani iwe kwenu! Karibuni nyumbani mwangu. Nitawapa mahitaji yenu yote, msilale katika uwanja huu wa mji.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mzee akawaambia, “Amani iwe kwenu! Karibuni nyumbani mwangu. Nitawapa mahitaji yenu yote, msilale katika uwanja huu wa mji.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha huyo mzee alisema, Amani Na iwe kwako; nitayakidhi mahitaji yenu yote; bora msikeshe nje.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo mzee akamwambia, “Amani iwe nanyi! Nitawapa mahitaji yote. Ila msilale huku uwanjani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mzee akamwambia: Tengemana tu! Yote unayoyakosa nitakupatia, usilale tu nje uwanjani!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha huyo mzee alisema, Na iwe amani kwako; lakini na haya yaliyokupungukia na yawe juu yangu mimi lakini usilale njiani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyo muzee akamwambia: “Amani ikuwe nanyi! Nitawapa mahitaji yote. Lakini musilale huku katika kiwanja.”