Judges 19:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wanaume hao hawakumsikiliza. Kwa hiyo Mlawi yule akamchukua suria wake na kumtoa kwao huko nje. Nao wakamchukua na kumnajisi usiku kucha mpaka asubuhi. Karibu na mapambazuko, wakamwacha aende zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wale wanaume hawakumsikiliza. Hivyo yule mwanaume akamtoa yule suria wake nje kwa wale watu, nao wakambaka na kumnajisi usiku kucha hadi asubuhi. Kulipoanza kupambazuka, wakamwachia aende.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini hao watu hawakukubali kumsikia; basi mtu huyo akamshika suria wake, na kumleta nje kwao; nao wakamjua, na kumtenda uovu usiku kucha hata asubuhi kisha kulipoanza kupambauka wakamwacha aende zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wanaume hao hawakumsikiliza. Kwa hiyo Mlawi yule akamchukua suria wake na kumtoa kwao huko nje. Nao wakamchukua na kumnajisi usiku kucha mpaka asubuhi. Karibu na mapambazuko, wakamwacha aende zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wale watu hawakumsikia. Hivyo yule mtu akamtoa yule suria wake nje kwa wale watu, nao wakambaka na kumnajisi usiku ule kucha mpaka asubuhi. Kulipoanza kupambazuka wakamwachia aende.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wale watu hawakumsikia. Hivyo yule mtu akamtoa yule suria wake nje kwa wale watu, nao wakambaka na kumnajisi usiku ule kucha mpaka asubuhi. Kulipoanza kupambazuka wakamwachia aende.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hao watu hawakumsikiliza; basi mtu huyo akamshika suria wake, na kumleta nje kwao; nao wakamjua, na kumtenda uovu usiku kucha hadi asubuhi kisha kulipoanza kupambazuka wakamuacha aende zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wanaume hao hawakumsikiliza. Kwa hiyo Mlawi yule akamchukua suria wake na kumtoa kwao huko nje. Nao wakamchukua na kumnajisi usiku kucha mpaka asubuhi. Karibu na mapambazuko, wakamwacha aende zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hao watu wakakataa kumsikia; ndipo, yule mtu alipomkamata suria yake, akamtoa nje kwao. Nao walipomjua wakamfanyizia mabaya usiku kucha mpaka asubuhi; kulipopambazuka, ndipo, walipomwachia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini hao watu hawakukubali kumsikia; basi mtu huyo akamshika suria wake, na kumleta nje kwao; nao wakamjua, na kumtenda uovu usiku kucha hata asubuhi kisha kulipoanza kupambauka wakamwacha aende zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wanaume hao hawakumusikiliza. Kwa hiyo Mulawi yule akamutwaa habara yake na kumutoa kwao kule inje. Nao wakamutwaa na kulala naye kwa kinguvu usiku kucha mpaka asubui. Karibu na mapambazuko, wakamwacha aende zake.