Judges 19:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana wa mwanamke huyo alipoamka asubuhi, alifungua milango ya nyumba, akatoka nje ili aendelee na safari. Ghafla akamkuta suria wake amelala chini mlangoni, mikono yake ikishika kizingiti cha mlango.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bwana wake alipoamka asubuhi na kufungua mlango wa nyumba na kutoka nje ili kuendelea na safari yake, tazama, yule suria wake alikuwa ameangukia penye ingilio la nyumba, mikono yake ikiwa penye kizingiti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wake akaondoka asubuhi, akaifungua milango ya nyumba, akatoka nje ili aende zake, na tazama, huyo mwanamke suria yake alikuwa ameanguka pale mlangoni pa nyumba, na mikono yake ilikuwa i pale kizingitini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana wa mwanamke huyo alipoamka asubuhi, alifungua milango ya nyumba, akatoka nje ili aendelee na safari. Ghafla akamkuta suria wake amelala chini mlangoni, mikono yake ikishika kizingiti cha mlango.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bwana wake alipoamka asubuhi na kufungua mlango wa nyumba na kutoka nje ili kuendelea na safari yake, tazama, yule suria wake alikuwa ameanguka pale penye ingilio la nyumba na mikono yake ikiwa penye kizingiti cha chini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bwana wake alipoamka asubuhi na kufungua mlango wa nyumba na kutoka nje ili kuendelea na safari yake, tazama, yule suria wake alikuwa ameanguka pale penye ingilio la nyumba na mikono yake ikiwa penye kizingiti cha chini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana wake akaondoka asubuhi, akaifungua milango ya nyumba, akatoka nje ili aende zake, na tazama, huyo mwanamke suria wake alikuwa ameanguka pale mlangoni pa nyumba, na mikono yake ilikuwa iko pale kizingitini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana wa mwanamke huyo alipoamka asubuhi, alifungua milango ya nyumba, akatoka nje ili aendelee na safari. Ghafla akamkuta suria wake amelala chini mlangoni, mikono yake ikishika kizingiti cha mlango.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana wake alipoinuka asubuhi, akaifungua milango ya nyumba; tena alipotoka, ashike njia ya kwenda zake, mara akamwona suria yake vivyo hivyo, alivyokuwa ameanguka mlangoni penye nyumba, mikono yake ikishika kizingiti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana wake akaondoka asubuhi, akaifungua milango ya nyumba, akatoka nje ili aende zake, na tazama, huyo mwanamke suria yake alikuwa ameanguka pale mlangoni pa nyumba, na mikono yake ilikuwa i pale kizingitini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wa mwanamuke yule alipoamuka asubui, akafungua milango ya nyumba, akatoka inje kusudi aendelee na safari. Kwa rafla akamukuta habara yake amelala chini mbele ya mulango, mikono yake ikishika kizingiti cha mulango.