Judges 19:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja, mumewe alikwenda kumtafuta; alikusudia kuongea naye vizuri na kumrudisha nyumbani kwake. Basi huyo mwanamume alikwenda pamoja na mtumishi wake na punda wawili. Basi yule mwanamke akampeleka ndani kwa baba yake, naye baba mkwe wake alipomwona akampokea kwa furaha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mume wake akaenda kumsihi arudi. Alienda na mtumishi wake na punda wawili. Yule mwanamke akamkaribisha nyumbani mwa baba yake, naye baba yake alipomwona akamkaribisha kwa furaha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha mumewe akainuka akamfuata, aseme naye kwa upendo, ili apate kumrudisha tena, naye alikuwa na mtumishi wake pamoja naye na punda wawili; huyo mwanamke akamkaribisha katika nyumba ya baba yake; naye baba yake alipomwona akafurahi kuonana naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja, mumewe alikwenda kumtafuta; alikusudia kuongea naye vizuri na kumrudisha nyumbani kwake. Basi huyo mwanamume alikwenda pamoja na mtumishi wake na punda wawili. Basi yule mwanamke akampeleka ndani kwa baba yake, naye baba mkwe wake alipomwona akampokea kwa furaha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mume wake akaenda kumsihi ili arudi. Alikwenda na mtumishi wake na punda wawili. Yule mwanamke akamkaribisha nyumbani mwa baba yake, baba yake alipomwona akamkaribisha kwa furaha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mume wake akaenda kumsihi ili arudi. Alikwenda na mtumishi wake na punda wawili. Yule mwanamke akamkaribisha nyumbani mwa baba yake, baba yake alipomwona akamkaribisha kwa furaha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha mumewe akaondoka akamfuata, aseme naye kwa upendo, ili apate kumrudisha tena, naye alikuwa na mtumishi wake pamoja naye na punda kadhaa; huyo mwanamke akamkaribisha katika nyumba ya baba yake; naye baba yake alipomwona akafurahi kuonana naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja, mumewe alikwenda kumtafuta; alikusudia kuongea naye vizuri na kumrudisha nyumbani kwake. Basi huyo mwanamume alikwenda pamoja na mtumishi wake na punda wawili. Basi yule mwanamke akampeleka ndani kwa baba yake, naye baba mkwe wake alipomwona akampokea kwa furaha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mumewe alipoondoka, akamfuata, aseme naye maneno ya kuugeuza moyo wake, apate kumrudisha; alikuwa anaye mtumishi wake na punda wawili. Yule kijana wa kike akamwingiza nyumbani mwa baba yake, naye baba yake alipomwona akafurahi kwa kukutana naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha mumewe akainuka akamfuata, aseme naye kwa upendo, ili apate kumrudisha tena, naye alikuwa na mtumishi wake pamoja naye na punda wawili; huyo mwanamke akamkaribisha katika nyumba ya baba yake; naye baba yake alipomwona akafurahi kuonana naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja, mume wake akakwenda kumutafuta. Alikusudia kuongea naye vizuri na kumurudisha kwa nyumba yake. Akakwenda pamoja na mutumishi wake na punda wawili. Basi yule mwanamuke akamupeleka ndani kwa baba yake, naye baba mukwe alipomwona akamupokea kwa furaha.