Judges 19:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya tano huyo mtu aliamka asubuhi, akitaka kuondoka. Lakini baba yake yule mwanamke akamwambia, “Kwanza upate nguvu kwa kula, ungoje alasiri, halafu uondoke.” Basi wote wawili wakala pamoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asubuhi ya siku ya tano, alipoamka ili aondoke, baba wa yule msichana akamwambia, “Jiburudishe nafsi yako. Ngoja hadi alasiri!” Kwa hiyo wote wawili wakala chakula pamoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akaamka asubuhi na mapema siku ya tano ili aende zake; na baba yake mwanamke akasema, Tuza moyo wako, tafadhali, ukae hata jua lipinduke; nao wakala chakula wote wawili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya tano huyo mtu aliamka asubuhi, akitaka kuondoka. Lakini baba yake yule mwanamke akamwambia, “Kwanza upate nguvu kwa kula, ungoje alasiri, halafu uondoke.” Basi wote wawili wakala pamoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asubuhi ya siku ya tano, alipoamka ili aondoke, baba wa yule msichana akamwambia, “Jiburudishe nafsi yako. Ngoja mpaka mchana!” Kwa hiyo wote wawili wakala chakula pamoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asubuhi ya siku ya tano, alipoamka ili aondoke, baba wa yule msichana akamwambia, “Jiburudishe nafsi yako. Ngoja mpaka mchana!” Kwa hiyo wote wawili wakala chakula pamoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akaamka asubuhi na mapema siku ya tano ili aende zake; na baba yake mwanamke akasema, Tunza moyo wako, tafadhali, ukae hadi jua litue; nao wakala chakula wote wawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya tano huyo mtu aliamka asubuhi, akitaka kuondoka. Lakini baba yake yule mwanamke akamwambia, “Kwanza upate nguvu kwa kula, ungoje alasiri, halafu uondoke.” Basi wote wawili wakala pamoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya tano akaamka na mapema, aende zake; lakini babake yule kijana wa kike akasema: Ushikize moyo wako, mkawilie, mpaka jua lipinduke. Wakala wao wawili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akaamka asubuhi na mapema siku ya tano ili aende zake; na baba yake mwanamke akasema, Tuza moyo wako, tafadhali, ukae hata jua lipinduke; nao wakala chakula wote wawili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya tano yule mutu akaamuka asubui, akataka kuondoka. Lakini baba ya yule mwanamuke akamwambia: “Kwanza upate nguvu kwa kula, ungoje mpaka jua litakaposhuka, halafu uondoke.” Basi wote wawili wakakula pamoja.